Homa kwa Mchanga Wa Umri Chini ya Miezi 3 na Mtoto wa Umri chini ya Mwaka 1.

Homa kwa Mchanga Wa Umri Chini ya Miezi 3 na Mtoto wa Umri chini ya Mwaka 1.

Homa kwa Mchanga Wa Umri Chini ya Miezi 3 na Mtoto wa Umri chini ya Mwaka 1.

Homa ni dalili ambayo huhusisha kuongezeka kwa Joto la Mwili wa Mtoto Mchanga, Joto la kuanzia 38⁰Centigrade au 100.4⁰ Fahrenheit kwenda juu humaanisha homa kwa Mtoto Mchanga.

Joto la kawaida kwa Mtoto Mchanga wa umri wa Siku 1 hadi Miezi Mitatu ni kati ya 36.5⁰C hadi 37.4⁰C, kwa kupima kwenye kwapa la Mtoto Mchanga.

Swali:
Kwa nini Homa kwa Mtoto Mchanga ni Joto kuanzia 38⁰C au zaidi?, wakati Joto la Mwili wa Kichanga kawaida ni kati ya 36.5⁰C hadi 37.4⁰C.

Jibu!
Maana ya Homa ni Joto la kuanzia 38⁰C au zaidi hii ni kutokana na kupima Joto la Kichanga kwenye njia ya haja kubwa ambayo ndio njia nzuri zaidi.

Njia za kupima Joto la Kichanga ni kama:

  1. Kupima Joto kwenye njia ya haja ya kubwa ya Kichanga (Ndio inayotakiwa).
  2. Kupima Joto kwenye Mdomo wa Kichanga.
  3. Kupima Joto la Kichanga Kwenye Sikio la Kichanga.
  4. Kupima Joto kwenye kwapa la Kichanga.

Kati ya hizo Njia zote njia ambayo huwa na majibu sahihi zaidi ni kupima Joto la Kichanga kwa Kuweka kipimo Joto kwenye njia ya haja kubwa ya Kichanga.

Joto la kawaida kwa Mtoto Mchanga lililopimwa kwenye njia ya haja kubwa ya Kichanga huwa kati ya 36.5⁰C -37.9⁰C.

Joto la kawaida kwa Mtoto Mchanga lililopimwa kwenye Kwapa la Kichanga huwa kati ya 36.5⁰C -37.4⁰C.

NB: Hivyo kiwango cha Joto la kawaida kwa Kichanga tajwa pale juu ni kwa kupima Joto la Kichanga kwenye kwapa la Kichanga.

🔥.Njia ya haja kubwa ni nzuri ila huwa na changamoto mbalimbali mfano: Kumuumiza Kichanga njia ya haja kubwa, Kuambukiza Magonjwa endapo utatumiwa bila kusafishwa na bila kuzingatia mazingira ya usafi na nk.

Joto la Kichanga linapokuwa kuwa chini ya 36.5⁰C huashiria kuwa Kichanga Joto lake liko chini kuliko kawaida vile vile Joto linapokuwa zaidi ya 37.5⁰C huashiria kuwa Joto lake liko juu kuliko kawaida ni Homa au amechemka.

Ongezeko la Joto/Kuchemka ambayo ni Homa huashiria kuwa Kichanga ana shida inayoendelea Mwilini mwake yawezekana kuna Maambukizi ya Vijidudu au shida nyingine.

VISABABISHI VYA HOMO KWA VICHANGA.
Yafuatayo ni Mambo ambayo yanaweza kupelekea Homa kwa Kichanga ambayo ni kama:

  1. Maambukizi ya Virusi mwilini mwa Kichanga (Kwenye mfumo wa hewa,Mfumo wa chakula, Mfumo wa Damu, Mfumo wa fahamu na nk)
  2. Maambukizi ya Vijidudu/Bacteria Mwilini mwa Kichanga (Kwenye mfumo wa hewa,Mfumo wa chakula, Mfumo wa Damu, Mfumo wa fahamu na nk)
  3. Aleji au kusisimuliwa kwa mfumo wa Kinga wa Mtoto Mchanga.
  4. Chanjo za kawaida kwa vichanga (haswa chanjo ya DPT= Dephtheria-Pertussis-Tetanus huchomwa kwenye paja la kushoto la Kichanga) na nk.

Dalili hii ya Homa ni vema kuichukulia Uzito kwa Vichanga hawa, kwa sababu wakati mwingine Vichanga huweza kuwa na dalili hii moja tu na pekee, ndiyo ambayo inaonesha kuwa Mtoto huyu ana Maambukizi ya Vidudu au changamoto inaendelea Mwilini mwake.

NB: Kichanga wa umri wa chini ya umri wa Miezi Mitatu (3) mwenye dalili hii ya Homa unatakiwa kumuwahisha hospitali kwa ajili ya vipimo na Matibabu bila kuchelewa.

Vichanga wa umri wa Miezi 3 kwenda juu au Watoto waliopo chini ya Mwaka mmoja huweza kuwa na dalili ya Homa pekee au huweza kuwa na Homa na dalili ambatanishi kama hizi zifuatazo:

  1. Kushindwa Kupumua/Kupumua haraka haraka/ Matunda ya pua kutanuka wakati wa kupumua/Sehemu ya chini ya kifua kuingia ndani.
  2. Kushindwa kunyonya/Kulia mara kwa mara/Kuto kula au kunywa.
  3. Kulia kwa Sauti kali.
  4. Kupunguza Mkojo au kulia wakati wa kukojoa.
  5. Utosi kuvimba kichwani.
  6. Kichanga kutapika.
  7. Kichanga kupata degedege na nk.

NB: Mzazi au Mlezi uonapo hizo dalili ni vema kumuwahisha mwanao hospitali bila kuchelewa hata mara moja ili akafanyiwe vipimo na Matibabu stahiki.

JINSI YA KUPUNGUZA HOMA YA KICHANGA NYUMBANI.

Wazazi walio wengi wanapoona Kichanga Joto lake limezidi 37.5⁰C na liko chini ya 38⁰C hukimbilia kumpa Kichanga Dawa za kupunguza Homa (Paracetamol au Panadol au Ibuprofen) kitendo hiki si kizuri kiafya kwa sababu Vichanga hawa Maini na Viungo vyao havija komaa vizuri, hivyo si vema kuwapa Madawa kiholela bila idhini ya Daktari au Pasipo kuandikiwa na Daktari badala yake mzazi unaweza kufanya Mambo haya kabla hujampeleka dispensari, Kituo cha Afya au Hospitali.

  1. Punguza nguo ulizomvisha Kichanga kama ziko nyingi ili awe wazi kwa ajili ya kupunguza Homa na mvishe nguo nyepesi.
  2. Mtoto ambaye yuko zaidi ya miezi 6 mpe maji ya kunywa kulingana na uhitaji wake, chini ya miezi 6 endelea kunyonyesha mara kwa mara.
  3. Tafuta kitambaa loanisha na maji ya Uvuguvugu mkande kande na kitambaa chenye unyevu kwenye paji la uso wake.
  4. Haraka mpeleke Dispensari, Kituo cha Afya au hospitali ya karibu kwa ajili ya Uchunguzi,vipimo na Matibabu stahiki kwa sababu Homa ni dalili siyo ugonjwa bali huashiria Ugonjwa/Shida fulani inaendelea Mwilini mwa Kichanga hivyo si vema kuwapa Dawa za kupunguza Homa endapo Joto liko kati ya 37.5⁰C hadi 38⁰C.

KUMBUKA:
Kuna mambo yanayoweza kumfanya Mzazi/Mlezi kumpa Dawa ya Homa Kichanga endapo kuna Mambo yafuatayo ili kuepuka changamoto kwa Kichanga wakati mnaelekea kituo cha Afya au hospitali;

  1. Inawezekana kuna umbali mrefu mpaka Dispensari, Kituo cha Afya au hospitali na Joto la Kichanga liko kuanzia 39⁰C au Zaidi.
  2. Kichanga alichomwa Chanjo (haswa DPT) ana Homa na Mzazi au Mama amewasiliana na kuruhusiwa na Daktari wako kuhusu kiwango cha Dawa ya kupunguza Homa.
  3. Umewasiliana na Daktari wako na amekuruhusu kiwango maalum cha dawa hiyo ya Homa.

©MAMA AFYA BORA

TUNA SISITIZA KUWA USIMPE DAWA YA HOMA KICHANGA (PARACETAMOL AU IBUPROFEN) BILA IDHINI YA DAKTARI BADALA YAKE WAHI HOSPITALI MAPEMA.

No comments.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *