Kujifungua Mtoto Mkubwa (Big Baby) Kilo 4 au Zaidi.
Mtoto Mkubwa (Macrosomia) ni Mtoto mchanga anayezaliwa na kilo 4 au zaidi, wakati mwingine Mtoto aliyeko Tumboni mwa Mjamzito huweza kuwa na kilo nyingi kuliko umri wa Mimba (Large for gestation age).
Hivi karibuni kuna taarifa zilitoka ya kwamba kuna Mtoto Mchanga aliyezaliwa na kilo 7.3Kg (Macrosomia) nchini Brazil, Mama yake Mbrazili mwenye Umri wa Miaka 42 na mwenye Ugonjwa wa Kisukari.
Kuna Mambo au Sababu tofauti tofauti ambazo zinaweza kupelekea Mjamzito kuwa na Mtoto Mkubwa Tumboni au Kujifungua Mtoto Mchanga mwenye Kilo 4 au zaidi, Sababu za Kujifungua Mtoto Mkubwa kuliko kawaida ni kama;
- Ugonjwa wa Kisukari cha muda mrefu kwa Mjamzito au Kisukari cha Ujauzito.
- Mama mwenye asili ya Uzito mkubwa au Kiriba Tumbo kabla ya kuwa Mjamzito BMI > 25Kg/M².
- Historia ya Kujifungua Watoto wakubwa zaidi ya kilo 4 kwa Mimba zilizopita.
- Mjamzito mwenye umri mkubwa zaidi ya Miaka 35.
- Mtoto jinsia ya Kiume.
- Kuzidisha au kupitiliza tarehe ya Matarajio, Mimba yenye Umri wa wiki 41 au zaidi.
- Kuongezeka Uzito kwa kasi kubwa katika kipindi cha Ujauzito.
- Mjamzito aliyewahi kujifungua zaidi ya mara Tatu katika kipindi cha maisha yake.
- Maji mengi yanayomzunguuka Mtoto tumboni mwa Mjamzito.
- Mjamzito aliyezaliwa akiwa na Uzito mkubwa zaidi na nk.
JINSI YA KUJUA KAMA UNA MTOTO KUBWA TUMBONI (MTOTO MWENYE KILO NYINGI TUMBONI).
Ili Mjamzito aweje kujua kuwa ana Mtoto Mkubwa Tumboni mwake anaweza kufanya baadhi ya vipimo na vile vile kutambua kwa kupitia dalili chache kama;
- Kupima Urefu Wima wa Tumbo,Mimba ifikishapo wiki 20 au wiki 24 kwenda juu huweza kuonesha Urefu wa Kimo cha Tumbo kuwa mkubwa zaidi kuliko umri wa Mimba katika Wiki, Tumbo kubwa bila Mapacha au Maji mengi yanayomzunguuka Mtoto hii huashiria una Mtoto mkubwa tumboni.
- Kufanya Ultrasound ambapo huweza kuonesha na kupima Uzito wa Mkadirio wa Mtoto aliyeko Tumboni mwa Mjamzito (EFW), endapo Mtoto aliyeko Tumboni ana Uzito wa Makadirio Mkubwa kuliko Umri wa Mimba hiyo huweza kuashiria kuwa anaweza kujifungua Mtoto Mchanga Mkubwa kuliko kawaida hapo badae.
- Dalili mfano kuongezeka kwa Uzito wa Mjamzito kwa kasi na haraka zaidi kuliko kawaida na kuwa na Tumbo kubwa kwa Mjamzito bila kuwa na Mapacha au Maji mengi yanayozunguka Tumboni.
MADHARA YA KUWA NA MTOTO MKUBWA TUMBONI MWA MJAMZITO.
Endapo Mjamzito una Mtoto Mkubwa Tumboni katika kipindi cha Ujauzito huweza kuleta Madhara haswa wakati wa kujifungua kwa Mjamzito na Mtoto Mchanga Mwenyewe, Madhara hayo ni kama;
Madhara ya kuwa na Mtoto Mkubwa kwa Mjamzito.
- Kujifungua kawaida kwa Upasuaji saidizi, kwa kutumia vifaa saidizi kama forceps au Vacuum.
- Kuchanika kwa Mlango wa Uzazi au Ukeni wakati wa Kujifungua kawaida.
- Kuongeza hatari ya kupoteza Damu nyingi baada ya kujifungua kutokana na mji wa Uzazi kutorudi kwa hali yake na kawaida.
- Kujifungua kwa Upasuaji.
- Kupata Uchungu pingamizi na kujifungua Mtoto aliyechoka zaidi.
- Kupasuka kwa Mshono kwa Mama ambaye aliye na Kovu moja au mawili kutokana na kujifungua kwa Upasuaji kwa Mimba zilizopita.
- Uchungu kuchukua muda mrefu zaidi kuliko kawaida.
Madhara kwa Mtoto Mchanga Mkubwa (Kilo 4 au zaidi).
- Kupoteza Sukari nyingi baada ya kuzaliwa haswa kwa wale wanaozaliwa kwa Mama zao wenye Ugonjwa wa Kisukari.
- Kuwa na hatari ya kuwa na Uzito Mkubwa zaidi Utotoni.
- Kukaa muda mrefu hospital na kuwa kwenye hatari ya kupata Magonjwa ambukizi hospitali.
- Gharama kuongezeka kwa wazazi na nk.
Jinsi gani ya kuzuia kuwa na Mtoto Mwenye Uzito Mkubwa Tumboni mwa Mjamzito
- Kuwahi kliniki na kufanyiwa vipimo mapema na kufuata utaratibu wa Kliniki.
- Matumizi mazuri ya Dawa za Kisukari ili kudhibiti athari za Sukari nyingi na Ugonjwa wa Kisukari.
- Kufanya mazoezi ya kutembea na shughuli ndogo ndogo kwa dakika 30 siku 5 za wiki kama Mimba haina shida yoyote.
KUMBUKA:
Wakati mwingine si rahisi kuzuia kuongezeka kwa Uzito wa Mtoto aliyeko tumboni mwa Mjamzito katika kipindi cha Ujauzito, ndio maana ili kupeuka changamoto za kutokana na Uzito Mkubwa wa Mtoto, Madaktari hushauri kujifungua kwa kufanyiwa Upasuaji kwa baadhi ya Wajawazito.
No comments.