KITOVU CHA MTOTO MCHANGA NYUMBANI, {JINSI YA KUTUNZA KITOVU CHA MTOTO MCHANGA.}

KITOVU CHA MTOTO MCHANGA NYUMBANI, {JINSI YA KUTUNZA KITOVU CHA MTOTO MCHANGA.}

KITOVU CHA MTOTO MCHANGA NYUMBANI, {JINSI YA KUTUNZA KITOVU CHA MTOTO MCHANGA.}

Kitovu cha Mtoto Mchanga ni Kovu lililopo sehemu ya katikati ya Tumbo la Mtoto Mchanga ambayo huwa ina bakia baada ya kukatwa kwa Mrija punde tu baada ya Mtoto Mchanga anapozaliwa Mrija unao muunganisha Mtoto na Kondo la nyuma anapokuwa Tumboni mwa Mama.

Mrija huo hukatwa dakika chache tu baada ya Mtoto Mchanga kuzaliwa na hubakia sehemu ndogo tu ya sentimita kama 2 tu ambapo huwa umebanwa na kibanio cha Kitovu ili kuzuia kutokwa Damu kwa Mtoto Mchanga.

Kitovu cha Mtoto Mchanga na Kovu lake ni muhimu kutunzwa katika mazingira ya usafi ili kiweze kupona vizuri bila kupata Maambukizi ya Vijidudu na kupona kwa wakati.

Kitovu cha Mtoto Mchanga hudondoka chenyewe na kupona siku 7 hadi siku 15 baada ya Mtoto Mchanga kuzaliwa. Kawaida Kovu na Mrija wa Kitovu uliobaki huwa na unyevu kidogo na huendelea kukauka kadiri muda unavyokwenda baada ya siku kadhaa huanza kubadilika rangi kuwa Nyeusi au Brown na mwisho wa siku mrija ulioshikwa na Kibanio cha Kitovu hudondoka wenyewe bila kutolewa.

Endapo Kovu na Mrija wa Kitovu uliobaki unatoa harufu mbaya, kutokwa Damu, Kuwa na unyevu usio wa kawaida au Maji maji yenye harufu, kuvimba au dalili yoyote ya hatari unatakiwa kwenda hospitali kwa ajili ya Uchunguzi.

Endapo Mabaki ya Mrija huo umedondoka na kumebaki na uwazi bila kufunga vizuri au endapo kitovu hakija dondoka baada ya wiki 2 tokea Mtoto Mchanga kuweza kuzaliwa unatakiwa kwenda hospitali kwa ajili ya uchunguzi zaidi na Matibabu.

NAMNA YA KUTUNZA KITOVU CHA MTOTO MCHANGA NYUMBANI

Mama mzazi au Mlezi Kuna Mambo unatakiwa kufanya ili kuhakikisha Kitovu Cha mwanao Mchanga kinakuwa katika Mazingira safi na Salama ili kuepuka Maambukizi, Mambo hayo ni kama;

  1. Usimwogesha Mtoto mchanga au kuloanisha kitovu kabla hakijadondoka au kupona kabisa.
  2. Msafisha mwanao kwa kumfuta tu kwa kitambaa safi cha Pamba ambacho kina unyevu kiasi tu baada ya kuloeshwa na Maji safi na salama .
  3. Unampomvalisha Pampasi Mtoto Mchanga ambaye Kitovu chake hakija anguka hakikisha isiguse eneo la Kitovu au Kibanio cha Kitovu ili kuepuka Maambukizi ya Vijidudu endapo pampasi imeloa na Mkojo.
  4. Kama una Pampasi kubwa sana hakikisha umekunja ili isiguse kitovu cha Mtoto Mchanga.
  5. Usiguse Kitovu cha Mtoto Mchanga kama Mikono yako haijaoshwa na Maji safi na salama.
  6. Usiguse Kitovu cha Mtoto Mchanga ambacho hakijadondoka na mikono yenye unyevu au ikiwa na Maji Maji.
  7. Usipake Dawa Yoyote kwenye kitovu pasipo maelekezo ya Daktari.
  8. Kama Kitovu kimedondoka na hakijafunga vizuri kabla ya kufanya chochote pata maelekezo ya Daktari.
  9. Hakikisha Kitovu cha mwanao ambacho hakijadondoka kisibanwe Sana na nguo au kuzibwa na Pampasi.

NAMNA YA KUTUNZA KITOVU CHA MTOTO MCHANGA NYUMBANI

Huhitaji kusafisha sehemu Kitovu mara kwa mara uwapo nyumba, ila unaweza kusafisha angalau kwa wiki mara moja tu, endapo kuna uhitaji wa kusafisha sehemu ya Kitovu cha Mtoto Mchanga ambacho hakijadondoka unaweza kufuata hatua zifuatazo,

Hatua za kusafisha Kitovu Cha Mtoto Mchanga uwapo nyumbani.

  1. Tumia maji safi na salama kunawa Mikono yako yote miwili.
  2. Andaa Chombo safi kitakachokuwa na Maji safi na Salama ya Uvuguvugu.
  3. Andaa Kitamba safi cha Pamba chenye unyevu kidogo.
  4. Tafuta sehemu yenye Joto pandisha juu nguo ya mwanao ili Tumbo liwe wazi na umlaze kwa Mgongo.
  5. Mlaze mwanao Chali au kwa Mgongo kwa ajili ya kuanza kusafisha mwanao.
  6. Chukua Kitambaa chako safi loeka sehemu ndogo ya Kitamba hicho kwenye maji ya uvuguvugu safi na salama halafu chuja maji pembeni ili kuondoa maji mengi kwenye Kitambaa ili kibaki na Unyevu kidogo tu.
  7. Safisha kwa kufuta kwa kuanzia kwenye mzizi wa kitovu kwa kuzunguuka taratibu na kwa uangalifu mkubwa.
  8. Safisha Kutokea kwenye mzizi kwenda pembeni na ukisha safisha katikati usirudie Tena kusafisha kati kati endelea kwenda pembeni.
  9. Tumia Kitambaa Kingine kisafi kausha kama kutakuwa na Unyevu umebaki mara baada ya kupitiisha kitamba cha kwanza.
  10. Tumia kitambaa cha pili kukausha kwa kugusa gusa taratibu pasipo kufuta kwa nguvu kuanzia kwenye Mzizi wa kitovu kuelekea pembeni taratibu.
  11. Hakikisha una msafisha haraka kwa Dakika 5 hadi10 na umvishe Mwanao nguo ili kuepuka kupoteza joto endapo akiwa uchi kwa muda mrefu.
  12. Hakikisha Kitovu cha Mwanao ambacho hakijadondoka ni kikavu muda wote, usiweke maji!.

KUMBUKA.

Huhitaji kumsafisha au kuogesha mtoto kila siku, unaweza ukamwogesha na kusafisha Mtoto Mchanga mara 2 au 3 kwa wiki, haina haja ya kuogesha mara kwa mara Mtoto mchanga chini ya Mwezi 1 kila siku au hata mara 2 kwa siku, Hakikisha una msafisha sehemu ya siri za mwanao kila anapojisaidia na kumkausha kwa Kitambaa safi ili kuhakikisha anakuwa mkavu mara kwa mara.

No comments.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *