Kwikwi Kwa Mtoto Mchanga

Kwikwi Kwa Mtoto Mchanga

Kwikwi Kwa Mtoto Mchanga

Kwikwi ni hali ambayo hutokea endapo Milango (Vocal Cords) iliyopo sehemu ya juu ya Koo la hewa inajifunga ghafla na haraka baada ya Msuli waa upumuaji (Diaflamu) kujikunja wakati mtu akiwa anaingiza hewa ndani, Hali hii hutokea kwa muda mfupi sana takribani sekunde 0.035 ambapo hutoa sauti ya HIC ndio iliyopelekea jina la Kwikwi kwa lugha ya Kingereza “Hiccup”.

Kwikwi hutokea zaidi kwa Watoto wa changa na wenye umri chini ya Mwaka 1 haswa wenye umri wa wiki chache hadi miezi kadhaa tokea kuzaliwa, hali hii huendelea kupungua au kutoweka kwa kadiri Mtoto Mchanga anapoongezeka umri, Kwikwi huweza kutokea kwa Mtoto Mchanga mara 4 hadi 60 kwa dakika moja.

JE SABABU ZA KWIKWI KWA MTOTO MCHANGA NI ZIPI?

Sababu kuu inayopelekea Kwikwi kwa Mtoto mchanga haijulikani vizuri lakini baadhi ya nadharia zinasema chanzo kikubwa cha Kwikwi kwa Mtoto Mchanga ni kujaa kwa Hewa au Gesi kwenye Tumbo la Mtoto Mchanga ambapo hupelekea msisimko na kujikunja kwa msuli mkubwa unao husika na Mambo ya Upumuaji na kupelekea Kwikwi kwa Mtoto Mchanga, Ziko sababu nyingine kama kuto kukomaa kwa mfumo wa fahamu wa Mtoto Mchanga na baadhi ya magonjwa, Zinafuatazo ni sababu ndogo ndogo zinazoweza kupelekea Kwikwi kwa Mtoto Mchanga,

  1. Mtoto Mchanga kuvuta gesi nyingi tumboni endapo ameshikizwa vibaya kwenye Chuchu ya ziwa la Mama.
  2. Kuvimbiwa kwa Kichanga kutokana na Kunyonya Maziwa mengi.
  3. Mtoto Mchanga kunyonya haraka haraka kwenye ziwa la Mama.
  4. Mtoto kushika vibaya chuchu ya kikombe kwa wale wanatumia Maziwa ya Kopo.
  5. Kuchanganya Maziwa ya Baridi na ya joto kwa wale wanaowapa Vichanga Maziwa ya Kopo.
  6. Kuchanganya Maziwa ya Kopo na Maziwa ya Mama kwa wale wanatumia Maziwa ya Kopo na Maziwa ya Mama kutokana na sababu mbalimbali.
  7. Kunyonyesha Mtoto akiwa analia.
  8. Kulia sana kwa Mtoto Mchanga huweza pelekea Kwikwi kwa Kichanga.
  9. Kunyonyesha Mtoto Mchanga akiwa na Njaa kali hupelekea kunyonya haraka haraka na kujaza gesi tumboni.
  10. Mama kutombeulisha na kumweka wima kwa dakika chache Kichanga mara baada ya Kunyonyesha.
  11. Baadhi ya Watoto huweza kuwa na Kwikwi mara kwa mara kutokana na Magonjwa ya kurudishwa kwa chakula nje kutokana na ulegevu wa Mlango wa koo la chakula (GERD) au Kiungulia (Heart burn)

JE NIFANYE NINI ILI KUPUNGUZA KUTOKEA KWA KWIKWI KWA KICHANGA?

Ukweli ni kwamba Kwikwi kwa Mtoto mchanga haina madhara yoyote na hutokea mara kwa mara kwa Mtoto mchanga anapokuwa na umri mdogo na huacha yenyewe kadiri umri wa kichanga unavyoongezeka, yafuatayo ni mambo unayoweza kufanya ili kuzuia kutokea kwa Kwikwi kwa kichanga,

  1. Mshikize Mtoto mchanga kwenye chuchu ya ziwa lako vizuri ili asivute gesi na kujaza tumboni.
  2. Mnyonyeshe Kichanga wako ashibe kiasi tu mara kwa mara ili asivimbiwe, kwa kawaida unaweza kunyonyesha kila baada ya masaa mawili(2) kwa kichanga aliyeko chini ya miezi 2 na kila baada ya masaa matatu (3) kwa kichanga aliye na umri wa miezi 2 kwenda juu.
  3. Endapo Mtoto mchanga ananyonya haraka haraka unaweza kumtoa kwenye ziwa baada ya sekunde kadhaa ukamrudisha tena kwenye Chuchu ya ziwa lako, hakikisha ananyonya pole pole.
  4. Mshikishikize Kichanga Vizuri kwenye Chuchu ya Kikombe kama una mnywesha maziwa ya Kopo.
  5. Epuka kuchanganya maziwa ya baridi na Joto kwenye baadhi ya vipindi endapo unampa maziwa ya Kopo.
  6. Epuka kuchanganya Maziwa ya Kopo na Maziwa ya Mama kwa Kichanga wako.
  7. Epusha Kichanga wako kulia sana, umtulize na ujue sababu inayopelekea kulia kwa Kichanga endapo analia.
  8. Epuka kunyonyesha Mtoto akiwa analia.
  9. Nyonyesha Mtoto mara kwa mara kuepuka kunyonya haraka haraka akiwa na Njaa kali na kumsafisha mara kwa mara.
  10. Mbeulishe Kichanga au Mpunguze Gesi na kumweka wima kwa dakika chache kila unapomaliza kunyonyesha.

Mama kumbuka unaweza ukamfanyia Kichanga wa Umri chini ya Mwaka 1 mambo yote tajwa hapo juu, lakini bado akaendelea kupata Kwikwi usiwe na wasiwasi, Mtoto Mchanga yoyote mwenye afya huweza kupata Kwikwi katika umri wake mdogo lakini kadiri umri unavyoongezeka hali hiyo hupungua yenyewe na kupona kabisa akifikisha mwaka 1 au zaidi, Ni hali ya kawaida sana!

JE NIFANYE NINI ILI KUPUNGUZA KWIKWI KWA MTOTO MCHANGA ALIYE NA KWIKWI?

Kwikwi kwa Mtoto Mchanga huweza kupungua na kutoeka yenyewe bila kupunguza wala kufanya chochote kwa kichanga, Lakini kuna baadhi ya mambo unaweza kufanya ili kupunguza Kwikwi kwa Kichanga endapo imekuwa kwa muda mrefu, Mambo hayo ni kama;

1. Mgonge gonge Kichanga Mgongoni kidogo kidogo kwa Kutumia Kiganja cha Mkono wako ukiwa umemuweka Kichanga wako kwenye bega au kumkalisha kitako au kumlaza tumbo kwenye Mapaja yako huku ukiwa umeinua kidogo sehemu ya kifua chake kwa muda wa dakika chache Kwikwi itaisha. Unaweza kutona picha jinsi ya kufanya kwa Kichanga wako hapo chini.

Jinsi ya kumpunguza Gesi Kichanga mwenye Kwikwi.
  1. Mpe Mtoto Mchanga Chuchu bandia ( Pacifier) awe ananyonya husaidia kupunguza Kwikwi kwa kichanga wako.
Chuchu Bandia (Pacifier).
  1. Mnyonyeshe Mtoto wako kidogo kidogo anapokuwa na Kwikwi, Hakuna shida hata ukinyonyesha Mtoto mchanga akiwa na Kwikwi.
  2. Muweke Mtoto Mchanga wima wakati wa kunyonyesha kipindi anapokuwa na Kwikwi.
Kunyonyesha Mtoto Mchanga akiwa Wima
  1. Muweke Mtoto Mchanga wima kwa dakika 15 hadi 20 baada ya kumaliza kumnyonyesha, kama unavyoona kwenye picha hapa chini.
Jinsi ya kumuweka Wima Mtoto Mchanga baada ya kunyonyesha.
  1. Mtoto chini ya Miezi 6 usimpe Gripe Water ili kupunguza Kwikwi, kwa sababu hakuna ulazima au Faida ya kutumia Gripe Water kupunguza Kwikwi labda kama Mtoto ana Umri zaidi ya Miezi 6 na kuendelea.
  2. Mtoto Mwenye Umri wa zaidi ya Miezi 6 unaweza kumpa Maji safi na salama kidogo kidogo kwenye Kijiko ili kupunguza Kwikwi kwa Kichanga wako.
  3. Mtoto Mchanga Anayepata Kwikwi mfululizo zaidi ya Saa 1 ni vema kumpeleka hospitali kwa ushauri wa Daktari.
  4. Mtoto ambaye anapata Kwikwi mara kwa mara na anabeua au kurudisha Maziwa na Chakula (GERD) au Kiungulia (Heartburn) ni vema umpeleke hospitali kwa ajili ya Matibabu.

USHAURI WA MAMA AFYA BORA KUHUSU KWIKWI KWA MTOTO MCHANGA HADI CHINI YA MWAKA MMOJA (1).

  1. Kwikwi kwa Mtoto Mchanga chini ya mwaka 1 na Mwenye afya bora ni hali ya kawaida kabisa, Mzazi uonapo Kwikwi kwa kichanga wako, usifadhaike na kuwa na msongo wa mawazo ni hali ya kawaida kabisa na hutoweka yenyewe baada ya dakika chache tu.
  2. Mtoto Mchanga anaweza kupata Kwikwi kwa kawaida mara 4 hadi 60 ndani ya dakika 1 na huweza kujirudia kila baada ya dakika kadhaa bila changamoto yoyote kiafya kwa Kichanga wako.
  3. Jifunze kunyonyesha vizuri Kichanga wako, kumweka Wima kwa dakika chache baada ya kunyonyesha na kumbeulisha ua kumpunguza gesi kila baada ya kumnyonyesha.
  4. Mtoto Mchanga anayepata Kwikwi mfululizo bila kupumzika ndani ya Saa 1 na kuendelea ni vema kumpeleka hospitali ili kupewa Matibabu.
  5. Mtoto ambaye anapata Kwikwi mara kwa mara na anabeua au kurudisha Maziwa na Chakula (GERD) au Kiungulia (Heartburn) ni vema umpeleke hospitali kwa ajili ya Matibabu.
Sikiliza Video ya Kwikwi kwa Mtoto Mchanga na Dr.Mwanyika.

No comments.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *