JE MJAMZITO ANAWEZA KUENDESHA GARI? (UENDESHAJI WA GARI KWA MJAMZITO)

JE MJAMZITO ANAWEZA KUENDESHA GARI? (UENDESHAJI WA GARI KWA MJAMZITO)

JE MJAMZITO ANAWEZA KUENDESHA GARI? (UENDESHAJI WA GARI KWA MJAMZITO)

Mjamzito unaweza kuendesha Gari kama kawaida wakati wa Ujauzito wako,ili mradi tu uko vizuri na unaweza kutumia gari kwa usalama. Mjamzito unaweza kuendesha gari Mwanzoni mwa Ujauzito mpaka Mwishoni mwa Ujauzito, hakuna kitu ambacho kinaweza kumzuia Mjamzito kuendesha Gari katika Ujauzito kama hana shida yoyote kiafya au katika Ujauzito wake.

Hakuna mwisho wa kuendesha Gari kwa Mjamzito au katika kipindi cha Ujauzito, labda endapo umeanza kuona au kuhisi dalili za uchungu ndipo unaweza kuacha kuendesha Gari hapo mpaka ujifungue ndipo utaanza kuendesha Gari yako.

Baadhi ya Wajawazito huwa na changamoto kiafya au katika Ujauzito wao ambazo hupelekea wao kushindwa au kuzuiliwa kuendesha Gari katika vipindi tofauti tofauti vya Ujauzito wao.

MAMBO YAFUATAYO HUWEZA KUPELEKEA MJAMZITO KUTOENDESHA GARI KATIKA UJAUZITO WAKE.

Mambo yafuatayo yanaweza kusababisha Mjamzito kuzuiliwa kuendesha Gari yake kutoka sehemu moja kwenda nyingine mfano: Kwenda kazini kwake katika kipindi cha Ujauzito, Japo hutofautiana kati ya Mjamzito Mmoja na Mwingine na vipindi tofauti tofauti vya Ujauzito.

  1. Mjamzito kuwa na hali ya Kichefuchefu au Kutapika mara kwa mara katika kipindi cha Ujauzito wake haswa Miezi 3 ya mwanzoni mwa Ujauzito.
  2. Mjamzito mwenye Kizunguzungu au kuishiwa nguvu mara kwa mara katika kipindi cha Ujauzito wake.
  3. Kutokwa Damu (Mimba kutishia kuharibika) katika kipindi cha Ujauzito hususani Mimba ambayo haijafikisha wiki 28 hapa Tanzania.
  4. Mjamzito mwenye Udhaifu wa Mlango wa uzazi ambapo huweza kusababisha Mimba kuharibika, kutoka au kujifungua kabla ya wiki 28 za Ujauzito.
  5. Mjamzito aliyeshonewa Mlango wa Uzazi ili kuzuia Mimba isitoke kabla ya wakati kwa sababu ya Udhaifu wa Mlango wa Uzazi.
  6. Mjamzito mwenye Dalili za hatari mfano, Chupa kupasuka, Presha kubwa sana katika Ujauzito,Homa kali katika Ujauzito na nk
  7. Kutokwa Damu (Kondo la Nyuma kujishikiza karibia na Mlango wa Uzazi) katika Miezi mitatu ya Mwishoni mwa Ujauzito yaani kuanzia wiki ya 28 kwenda juu.
  8. Mjamzito mwenye Maumivu makali ya Nyonga, Tumbo au Miguu katika kipindi chote chote cha Ujauzito.
  9. Mjamzito mwenye Tumbo kubwa mfano; Mjamzito mwenye Mapacha, Maji mengi Tumboni na nk ambapo huweza kupelekea Mjamzito kujisikia vibaya katika kipindi cha Ujauzito na kushindwa kuendesha Gari.
  10. Mjamzito aliyeandikiwa na Daktari kupumzika kitandani katika kipindi fulani cha Ujauzito wake (Bed rest) kwa sababu ya shida fulani katika Ujauzito wake.

KUMBUKA:

Mjamzito kama unasifa za kuendesha Gari na unaweza kuendesha Gari yako ni vema kuhakikisha unavaa mkanda vizuri na kufuata tahadhari zote za barabarani ili kuepuka Ajari za barabarani katika kipindi chako cha Ujauzito. Unaweza kuona picha hapo chini jinsi ya kuvaa mkanda.

Jinsi Mjamzito anavyotakiwa Kuvaa Mkanda akiwa kwenye Gari na anapoendesha gari yake.
Unaweza kusikiliza video kuhusu Mjamzito kuendesha gari katika kipindi cha Ujauzito.

No comments.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *