MATUMIZI YA ASALI KWA MJAMZITO NA FAIDA ZAKE? {TAHADHARI ZA ASALI KWA MJAMZITO}.

MATUMIZI YA ASALI KWA MJAMZITO NA FAIDA ZAKE? {TAHADHARI ZA ASALI KWA MJAMZITO}.

MATUMIZI YA ASALI KWA MJAMZITO NA FAIDA ZAKE? {TAHADHARI ZA ASALI KWA MJAMZITO}.

Asali ni Mojawapo la zao litokanalo na nyuki, Mwanadamu hutumia Asali katika matumizi mbalimbali, baadhi ya watu hutumia Asali kwa ajili ya kukausha na kuponya vidonda lakini pia sayansi inathibitisha hili kwamba Asali huweza kutumika kutibu vidonda, vile vile Asali hutumika kuongeza kinga ya mwili wa mwanadamu kwa kuua bakteria mbalimbali katika mwili na hutumika kama antioxidanti vile vile Asali hutumika kama Dawa ya kifua na Magonjwa mbalimbali, Asali huweza kutumiwa na watu wote isipokuwa watoto wadogo walio na umri chini ya mwaka mmoja vile vile Asali hutakiwa kutumiwa kwa tahadhari kubwa kwa akina Mama wajawazito.

Mjamzito anaweza kutumia Asali bila shida yoyote iwe Asali mbichi au Asali isiyo mbichi huweza kutumika katika kipindi chote cha Ujauzito bila kuleta athari zozote kwa Mjamzito. Kuna baadhi ya tafiti zinaonesha kwamba kuna baadhi ya Asali hususani Asali mbichi huweza kuwa na kiwango kidogo cha Mayai au Mbegu za vijidudu aina ya Clostridium ambapo endapo Mjamzito atatumia Asali ambayo ilikuwa na Mayai ya Vijidudu hao huweza kuleta changamoto endapo wakifanikiwa kuzaliana na kuingia kwenye mfumo wa damu moja kwa moja kwenda kwenye baadhi ya sehemu ya mfumo wa fahamu na kusababisha kupooza kwa sehemu husika,

Japo ni mara chache sana kwa sababu kinga ya Mama Mjamzito huweza kuzuia ukuaji wao. Hata kama Mayai ya Vijidudu hao yakiweza kutotoa na kuzalisha Vijidudu hawana uwezo wa kwenda kwa mtoto kwa kupitia Kondo la nyuma.

Asali haifai kupewa Mtoto mwenye umri wa mwaka mmoja au chini ya mwaka mmoja kwa sababu kinga zao huwa ziko chini sana endapo Vijidudu hao wakiweza kufika Tumboni mwa Mtoto huweza kuzaliana bila kuzuiliwa na kinga ndogo ya Mtoto na huweza kupelekea kupooza baadhi ya viungo na sehemu mbalimbali za mwili kwa sababu huweza kuathiri mfumo wa fahamu wa mtoto Mdogo.

ASALI HUWEZA KUTUMIKA KWA MJAMZITO BILA SHIDA YOYOTE ILE.

Mjamzito anayetumia Asali kwa siku vijiko 3 hadi 5 huweza kupata faida zifuatazo:

  1. Kuongeza kinga ya mwili, Asali huwa na antioxidants vile vile huweza kuua baadhi ya Bakteria wabaya mwilini mwa Mjamzito hivyo huongeza kinga ya Mjamzito.
  2. Huongeza nguvu kwa Mjamzito, unapotumia Asali huwa na sukari ambayo huweza kuongeza nguvu kwa Mjamzito hususani wajawazito ambao huwa na hali ya kuchoka choka.
  3. Huweza kupunguza kiungulia kwa Mjamzito. Baadhi ya Wajawazito huwa na Kiungulia au Vidonda vya Tumbo hivyo matumizi ya Asali ktk kipindi cha Ujauzito huweza kupunguza maumivu ya kiungulia au kuponya vidonda vya tumbo.
  4. Hupunguza na kutibu mafua na donda koo. Mjamzito ambaye anapata mafua ya aleji mara kwa mara endapo akiwa anatumia Asali mara kwa mara huweza kumtibu mafua na donda koo katika kipindi cha Ujauzito.
  5. Asali pia huweza kupunguza kukosa usingizi ktk kipindi cha Ujauzito.

KUMBUKA:

  1. Mjamzito unapotumia Asali usichanganye kwenye maji ya Moto kwa sababu unaweza kupunguza viini lishe hai na vimeng’enyishi vilivyomo kwenye Asali ambavyo ni muhimu sana kwenye mwili wa mama mjamzito.
  2. Mjamzito usichanganye Asali na Baadhi ya Vitamini C au D hii huweza kupelekea muingiliano na kufanya Vitamini zisifanyekazi vizuri katika Mwili wako.
  3. Mama usimpe Mtoto mwenye umri wa mwaka mmoja na chini ya mwaka mmoja Asali huwa na madhara makubwa sana.
Sikiliza video ya faida ya matumizi ya Asali kwa Mjamzito

Response to "MATUMIZI YA ASALI KWA MJAMZITO NA FAIDA ZAKE? {TAHADHARI ZA ASALI KWA MJAMZITO}."

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *