DALILI ZA MTOTO KUGEUKA TUMBONI MWA MJAMZITO {CEPHALIC PRESENTATION}.

DALILI ZA MTOTO KUGEUKA TUMBONI MWA MJAMZITO {CEPHALIC PRESENTATION}.

DALILI ZA MTOTO KUGEUKA TUMBONI MWA MJAMZITO {CEPHALIC PRESENTATION}.

Mtoto kugeuka (Cephalic Presentation) maana yake Nini?
Mtoto kugeuka ni vile Mtoto anapokuwa amegeuza kichwa chini kwenye Nyonga ya Mjamzito na pia Sura ya Mtoto kuangalia nyuma na chogo cha kichwa kuwa sehemu ya mbele au kwenye kinena cha Mwanamke Mjamzito.

Wajawazito 90 kati ya 100 Watoto wao hugeuza kichwa chini na sura kugeuzia nyuma (Occipital Anterior Position) hii ni kawaida kabisa na ndio inavyotakiwa ili Mjamzito aweze kujifungua kawaida vile vile Wajawazito 5 hadi 10 kati ya Wajawazito 100 wanaobaki wao Watoto wao hugeuza kichwa chini na sura kuwa mbele yaani Mtoto ana mchungulia Mama yake 😄😄😄 (Occipital Posterior Position) hawa huweza kujifungua kwa njia ya kawaida au wakafanyiwa Upasuaji endapo Uchungu hauendi ipasavyo.

Mtoto huanza kugeuka ktk Ujauzito Mimba inapofikisha wiki 20 hadi kabla ya Wiki 36 au Miezi 5 hadi Miezi 9 kasoro yaani kabla ya Wiki 37 na kuendelea.

Tafiti zinaonesha kwamba Wajawazito 75 kati ya Wajawazito 100 mpaka kufikia wiki ya 28 huwa tayari watoto wamegeuka tayari hivyo mpaka kufikia wiki 37 na zaidi ni wajawazito 3 tu kati ya Wajawazito 100 ambao Watoto huwa hawajageuka (Breech Presentation)

DALILI ZA MTOTO ALIYEGEUKA TUMBONI MWA MJAMZITO.
Dalili ambazo Mjamzito anaweza kuhisi endapo Mtoto ameshageuka ni kama;

  1. Kuhisi mtikisiko au Mtoto kucheza zaidi sehemu ya juu ya kitovu au Maeneo ya Mbavu.
    Endapo Mtoto amegeuka na amegeuza sura nyuma na chogo mbele (Occipital Anterior Position) Mjamzito atasikia Mtoto anacheza zaidi juu ya kitovu na maeneo karibia na Mbavu hii ni kutokana na Miguu yake kuwa maeneo hayo.
  2. Kuhisi mtikisiko au Mtoto kucheza zaidi sehemu ya kitovu au sehemu ya kati na mbele ya Tumbo la Mjamzito.
    Hii hutokea endapo Mtoto ameshageuka ila amegeuza sura mbele ya Nyonga na chogo iko nyuma ya Nyonga (Occipital Posterior Position) kwa baadhi ya Wajawazito wachache.
  3. Kuhisi Mgandamizo au Presha zaidi kwenye Nyonga, hii huweza kutokea kwa baadhi ya Wajawazito wanaweza kuhisi hivyo endapo mtoto amegeuka na ameshuka kwenye Nyonga ya Mjamzito.
  4. Kuhisi mvutiko au kuvuta kwenye Nyonga hii huweza kuashiria Mtoto amegeuka na ameshuka kwenye Nyonga hususani Mimba ya Miezi Mitatu ya mwishoni.
  5. Mapigo ya Moyo ya Mtoto kusikika sehemu ya chini ya Tumbo yaani chini ya kitovu inawezekana upande wa kushoto au upande wa kulia endapo Mjamzito atasikilizwa mapigo ya Moyo ya Mtoto aliyeko Tumboni mwake.

NB: Baadhi ya Wajawazito walio wengi huweza kuhisi Mtoto anacheza chini ya kitovu au upande wa kushoto na kulia ktk Ujauzito wao na Mtoto huyo akawa amegeuka tayari inawezekana ameshuka kwenye Nyonga ndio maana anacheza chini ya kitovu au upande wa kushoto au kulia tofauti na Dalili zinavyoelezea pale juu , usijali kama unachanganyikiwa unaweza kwenda hospitali, Kituo Cha Afya au Zahati na Mkunga, Nesi au Daktari akakusaidia kujua mkao wa Mtoto kwa njia za kitalamu na uhakika zaidi.

JINSI YA KUJUA MTOTO AMEGEUZA KICHWA CHINI AU MKAO WA MTOTO KITALAMU.
Madaktari au wahudumu wa Afya huweza kukusaidia kujua Mkao wa Mtoto aliyeko Tumboni mwako kwa kufanya haya:

  1. Kuchunguza au Kukagua Tumbo la Mjamzito (Leopold maneuvers), Ambapo Nesi, Mkunga au Daktari hukagua Tumbo lako na kujua Mtoto wako aliyeko Tumboni amekaaje na amegeuka au lah hii huleta majibu sahihi kwa 99% japokuwa hutegemeana na Ujuzi wa huyo mhudumu wa Afya.
  2. Kufanya Ultrasound, Baadhi ya Wajawazito endapo watafanya ultrasound huonesha Mtoto aliyeko Tumboni mwao amegeuka au mkao wake na huwa na uhakika au usahihi wa 100%.

KUMBUKA
Kama Mimba yako haijafikisha wiki 36 na Mtoto hajageuka basi usihofu Mtoto atageuka tuu, Kwa kawaida Mtoto atakuwa ametanguliza makalio endapo Mimba imefikisha wiki 36 au zaidi na Mtoto hajageuka bado.

Sikiliza video ya Mtoto kugeuka Tumboni kwa Mjamzito

Response to "DALILI ZA MTOTO KUGEUKA TUMBONI MWA MJAMZITO {CEPHALIC PRESENTATION}."

  • Kufunga kwa nyonga na kuuma chini ya kitovu. Huashilia mtoto tayari kageuka au bado?. Lakini hali hiyo husababisha na nini?

  • “Kama Mimba yako haijafikisha wiki 36 na Mtoto hajageuka basi usihofu Mtoto atageuka tuu”, je akiwa na zaidi ya wiki 37 na bado hajageuka,atageuka? Nini cha kufanya? Na madhara yake ni yapi endapo hata geuka?

  • Habari je kama mtoto amegeuka kunauwezekano akarudi kama mwanzo kutanguliza makalio au akishageuka ndiyo basi

  • Doctor nna Mimba Ya Miez 7 lakn Mtoto ameshageuk ila hachez Sana Mama Zaman Shida Iko wap Maana Naogopa Zaman Nlizoea Mashuti Saiv Namskia Chini Ya Kitovu Tuu

  • Samahani me ninamimba ya miezi minne lakini Mara nyingi tumbo unishika sana chini ya kitovu na mtoto anacheza chini ya kitovu yaan tumbo limevimba zaidi chini ya kitovu na kuna wakati nkikaa nkija kuinuka nyonga zinashika unaweza nipa ufahamu juu ya hilo please

  • Habari mm nina mimba ya miezi 8 wakati mwengine mtoto anakaza ya kama anasukuma tumbo inapelekea kuhc maumivu je nikawaida nijuze please

  • Ikiwa mimba in a wiki32 na kuanzia asubuh tumbo linauma sana kam uchungu na kuharisha je ni kuashiria nini kam tumbo linauma sana kisha haliponi linakata kidogo kisha maumiv yanarud tena

  • Leave a Reply

    Your email address will not be published. Required fields are marked *