SABABU ZA KUCHELEWA KUJIFUNGUA KWA MJAMZITO HIZI HAPA.

SABABU ZA KUCHELEWA KUJIFUNGUA KWA MJAMZITO HIZI HAPA.

SABABU ZA KUCHELEWA KUJIFUNGUA KWA MJAMZITO HIZI HAPA.

Mjamzito unatakiwa kujifungua wiki ya 37 hadi wiki ya 42 kwa tafsiri nyingine hiyo ndio Miezi 9, japokuwa kwa hesabu za kawaida wiki 42 ni sawa na Miezi 10 na wiki 2, ukizidisha wiki 43 hiyo huweza kuleta changamoto kwa Mtoto au Mama Mjamzito wakati wa kujifungua au kumpoteza Mtoto

Iko sababu moja kuu ambayo inapelekea Mjamzito achelewe kujifungua nayo ni :

Kusahau Hedhi ya mwisho ilipoanzia kabla ya kupata Mimba hii hupelekea kushindwa kujua tarehe ya matarajio na umri Mimba yake.

Unaweza kujua umri wa Mimba yako na Tarehe ya Matarajio kwa njia mbalimbali mfano:

  1. Kutumia Hedhi ya mwisho kabla ya kupata Mimba/Ujauzito.
  2. Kuhesa kutokea kipindi ambacho Mjamzito anaanza kusikia Mtoto anaanza kucheza Tumboni mwa Mjamzito.
  3. Kutumia ultrasound ya mwanzoni mwa Miezi Mitatu ya mwanzoni mwa Ujauzito na nk.

Sababu nyingine zinazoweza kupelekea Mjamzito kuchelewa kujifungua hazijulikana au bado hazijafahamika, Isipokuwa kuna mambo ambayo yanaweza kuhatarisha Mjamzito kuchelewa kujifungua.

Vihatarishi vinavyopelekea Mjamzito kuchelewa kujifungua ni kama;

  1. Mimba ya kwanza au Mjamzito anayebeba Ujauzito kwa mara ya kwanza katika maisha yake.
  2. Mimba au Mjamzito ambaye amebeba Mtoto jinsia ya Kiume Tumboniumboni.
  3. Mjamzito ambaye mimba ya kwanza alichelewa kujifungua huweza kuchelewa kujifungua Mimba ya pili kwa 27% au Mimba ya tatu kwa 39%.
  4. Mjamzito mwenye Uzito mkubwa wa kupindukia BMI ya 30Kg/M² au zaidi.
  5. Mjamzito ambaye wakati kuzaliwa yeye mwenyewe alichelewa kuzaliwa pia huweza kuchelewa kujifungua.
  6. Mjamzito anaweza kurithi kuchelewa kujifungua kutoka kwa wazazi wake au kizazi kingine.

Response to "SABABU ZA KUCHELEWA KUJIFUNGUA KWA MJAMZITO HIZI HAPA."

  • Nimekueelewa maana mm mtoto wa kwanza nilijifungua na 41 na huyu wa pili sa hv niko 40 bado cjajifungua, hivi kuna namna ya kuepukana na hii hali ya kujifungua kwa kuchelewa?? Maana inachosha kwakweli

    • Hapo kikubwa endelea kufanya mazoezi ya kutembea tembea kama huna shida yoyote inayokufanya usifanye mazoezi ya kutembea tembea na pia tumia chai ya Rangi kunywa ikiwa ya moto moto sawa eeh, jitahidi na kumwomba Mungu pia.

  • Leave a Reply

    Your email address will not be published. Required fields are marked *