MJAMZITO UNATAKIWA KUFANYA ULTRASOUND MARA NGAPI NA LINI KTK UJAUZITO WAKO?

MJAMZITO UNATAKIWA KUFANYA ULTRASOUND MARA NGAPI NA LINI KTK UJAUZITO WAKO?

MJAMZITO UNATAKIWA KUFANYA ULTRASOUND MARA NGAPI NA LINI KTK UJAUZITO WAKO?

Kulingana na ACOG Mwanamke Mjamzito anatakiwa kufanya Ultrasound angalau Mara mbili katika kipindi chote cha Ujauzito endapo Mimba yake haina shida yoyote!

Mjamzito ambaye Mimba yake inachangamoto fulani mfano; kutokwa Damu ktk Kipindi Cha Ujauzito, Presha ya Ujauzito, Kisukari cha Ujauzito, kutokwa Damu Miezi Mitatu ya Mwishoni mwa Ujauzito na nk,anaweza kufanya Ultrasound zaidi ya Mara mbili.

Mjamzito anatakiwa kufanya Ultrasound ya kwanza au kwa Mara ya kwanza Mimba inapokuwa chini ya Wiki 14 yaani miezi mitatu ya mwanzoni mwa Ujauzito.
Lakini pia atafanya Ultrasound ya Pili au kwa Mara ya Pili Mimba ikifikisha Kati ya wiki 18 hadi wiki 22.

Umuhimu wa kufanya Ultrasound ya kwanza au Mara ya kwanza Mimba ikiwa katika Miezi Mitatu ya mwanzoni mwa Ujauzito yaani chini ya wiki 14.
Miezi Mitatu ya mwanzoni mwa Ujauzito Ultrasound itakusaidia kujua Mambo kama:
1. Umri wa Mimba ulio sahihi zaidi(EDD or EDC)
2. Kuhakikisha kama kweli una Mimba
3. Kuhakikisha kama Mimba yako iko kwenye mji wa Uzazi na siyo nje ya Mji wa Uzazi (Ectopic pregnancy)
4. Kuhakikisha kama kweli Mtoto Yuko hai kwa kuona Mapigo ya Moyo ya Mtoto hususani Ultrasound ikifanyika Mimba inapokuwa na Wiki 7 kwenda juu (Fetal cardiac activity).
5. Kuhakikisha kama Una Mimba ya Mtoto Mmoja au Mapacha na nk.

Umuhimu wa kufanya Ultrasound ya pili au Mara ya Pili Mimba ikiwa katika Miezi Mitatu ya katikati mwa Ujauzito, yaani Mimba ikiwa umri wa kati ya wiki 18 hadi wiki 22.
Miezi Mitatu ya kati ya Ujauzito ultrasound itakusaidia kujua Mambo kama:
1. Viungo vya Mtoto viko sawa au lah(Fetal anatomy).
2. Uwingi wa maji yanayomzunguuka Mtoto(Amniotic fluid index).
3. Eneo lilipojishikiza Kondo la Nyuma(Location of Placenta).
4. Jinsi ya Mtoto aliyeko Tumboni mwa Mjamzito(Sex of the fetus).
5. Ulemavu wa Mtoto (Fetal anomaly) na nk

Kumbuka:
Endapo Mimba yako inachangamoto mfano;
1. Udhaifu wa Mlango wa Uzazi/Cervical incompetency.
2. Mimba kutishia kutoka/Threatened abortion.
3. Presha ya Ujauzito/ Gestational induced hypertension/Pre-eclampsia au Presha ya muda mrefu/Chronic/Essential Hypertension.
4. Mtoto kufia Tumboni au Mimba kuharibika mara kwa mara (BOH).
5. Kisukari cha Ujauzito/Gestational Diabetes
6. Kutokwa Damu katika Miezi Mitatu ya Mwishoni mwa Ujauzito (APH) na nk.
Hizo sababu huweza kupelekea Mjamzito kufanya Ultrasound zaidi ya Mara mbili katika kipindi cha Ujauzito.

Kumbuka:
Ultrasound haina Madhara yoyote kwa Mjamzito ila hutakiwi kufanya kiholela pasipo sababu ya msingi.!

Response to "MJAMZITO UNATAKIWA KUFANYA ULTRASOUND MARA NGAPI NA LINI KTK UJAUZITO WAKO?"

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *