MADHARA YA SODA KWA MJAMZITO

MADHARA YA SODA KWA MJAMZITO

MADHARA YA SODA KWA MJAMZITO

Unywaji Soda kwa Mjamzito ambao usio wa mara kwa mara hauna shida yoyote kwa Mjamzito asiye na Ugonjwa wa Kisukari au Presha!.

Unywaji wa Soda wa mara kwa mara au kila siku katika kipindi cha Ujauzito hata kama Mjamzito hana Magonjwa ya Kisukari au Presha huweza kupelekea Mtoto aliyeko Tumboni kuja kupata Shida ya Pumu hapo badae katika maisha yake.
Kuna baadhi ya Soda huwa na Caffeine kiwango cha 35mg hadi 55mg ndani yake ambapo Caffeine huwa na madhara endapo Mjamzito atazidisha kiwango cha zaidi ya 200mg kwa siku ambapo Caffeine huweza kupenya na kuingia kwa Mtoto kupitia Kondo la nyuma na kuleta athari kwa Mtoto aliyeko Tumboni mfano: Kujifungua Mtoto mwenye Uzito chini ya 2.5kg au kujifungua kabla ya wakati wa Kujifungua(Chini ya Wiki 37).

Soda ambazo hazina Caffeine huweza kupelekea ongezeko la Uzito zaidi kwa Mjamzito ambao huleta changamoto katika kipindi cha Ujauzito na wakati wa kujifungua, hivyo pia haifai kunywa Soda aina yoyote mara kwa mara au kila siku katika kipindi cha Ujauzito.

Mjamzito mwenye Ugonjwa wa Kisukari(Gestational Diabetes / DM type 1/2) au Mwenye Dalili za mwanzoni za kuelekea kupata Ugonjwa wa Kisukari (Pre-Diabetes) haruhusiwi kabisa kutumia Soda katika kipindi chochote cha Ujauzito kwa sababu huweza kupelekea Ongezeko kubwa la Sukari mwilini mwake na kuleta athari kwake na Mtoto aliyeko Tumboni. Mfano Mtoto kuwa na zaidi ya kilo 4 kipindi cha Kujifungua na kupelekea kujifungua kwa njia Upasuaji na Mtoto kuweza kuwa kwenye hatari ya kupungukiwa kwa Sukari haraka Mwili mwake baada ya Kuzaliwa hivyo hutakiwa kuwekwa kwenye chumba cha joto ili kuongezewa Maji yenye Sukari kwa muda fulani.

Mjamzito mwenye Presha ya Muda Mrefu (Chronic/Essential Hypertension) au Presha ya Ujauzito (Gestational Hypertension) endapo atatumia Soda zenye Caffeine huweza kupelekea ongezeko kubwa la Presha na mapigo ya Moyo kwenda mbio hivyo si vema kutumia Soda hizo huweza kupelekea changamoto katika Ujauzito wake na Presha au Shinizo kubwa la Damu yake(Hypertension).

Mjamzito yeyote haruhusiwi kutumia Vinywaji vyenye Sukari nyingi kwa sababu tafiti zinaonesha kwamba Wajawazito wanaotumia zaidi Vinywaji vyenye Sukari nyingi huweza kupelekea Mtoto atakaye zaliwa kuwa Upungufu wa uelewa na Upungufu wa jinsi ya kutamka na Shida ya Pumu(Asthma) katika maisha yake ya badae,

JE MJAMZITO AKINYWA SODA ZA DIET HUPATA MADHARA?
Utumiaji wa Soda za Diet usio wa mara kwa mara hauna shida yoyote kwa Mjamzito.

Utumiaji mbaya au zaidi ya Soda za Diet 4 kwa siku katika kipindi cha Ujauzito huweza kupelekea baadhi ya madhara kwa Mjamzito mfano; Kujifungua Mtoto kabla ya wakati wa kujifungua hivyo huweza kupelekea Mtoto kuwekwa kwenye chumba cha Joto kwa muda mrefu au Mtoto kupata Changamoto mbalimbali kutoka na Kuzaliwa kabla ya wakati.
Hivyo si vema kutumia Soda za Diet zaidi ya Soda 4 kwa siku huweza kupelekea changamoto hizo.

JE UNATAKIWA KUNYWA VITU GANI KATIKA KIPINDI CHA UJAUZITO?.

  1. Maji safi na Salama.
    Mjamzito unatakiwa kunywa Maji safi na Salama angalau Lita 1.5 hadi Lita 2 kila siku, Unywaji Maji huweza kuongezea Maji mwilini na pia hupunguza changamoto za Ujauzito mfano, kupunguza kupata Choo kigumu.
  2. Juisi ya Matunda na Mboga Mboga.
    Mjamzito unaweza kunywa Juisi ya Matunda au Mboga Mboga ya kiasili iliyoandaliwa katika Mazingira ya Usafi wa hali ya juu, Juisi ya Matunda huweza kuongeza Maji mwilini mwako, Vitamini na Madini mbalimbali katika kipindi chako cha Ujauzito bila kuathiri Afya ya Mtoto aliyeko Tumboni mwako.
  3. Chai ya rangi.
    Mjamzito unaweza ukatumia kiasi kidogo cha chai angalau kikombe kimoja cha chai husaidia kuchangamsha mwili wako, lakini kwa Mjamzito ambaye anakaribia kujifungua huweza kuongeza Uchungu wa Kujifungua, usinywe chai nyingi katika kipindi cha Ujauzito kwa sababu huweza kuwa na kiasi kingi cha Caffeine ambayo huweza kuleta athari kwa Mtoto aliyeko Tumboni mwako.

No comments.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *