JE ULTRASOUND INA MADHARA KWA MJAMZITO AU MTOTO ALIYEKO TUMBONI?

JE ULTRASOUND INA MADHARA KWA MJAMZITO AU MTOTO ALIYEKO TUMBONI?

JE ULTRASOUND INA MADHARA KWA MJAMZITO AU MTOTO ALIYEKO TUMBONI?

ULTRASOUND(SONOGRAM);
Ni Kifaa au Mashine ambayo hutumika kuonesha Taswira au Picha ya Sehemu Fulani ya Mwili wa Binadamu ambayo imeathiriwa au yenye Shida fulani ambapo wa Huduma wa Afya huhitaji kujua na kuona Hiyo sehemu Husika, Kifaa hiki hutengeneze Picha au Taswira ya Sehemu Fulani kwa kutengeneza Mawimbi ya Sauti ambayo huelekezwa kwenye sehemu Husika katika Mwili wa Mwanadamu na Kuaksiwa kwa Mawimbi hayo ya Sauti ndipo hutengeneze Picha Mfano Picha Ya; Mimba Ndani ya Mji wa Uzazi, Mji wa Uzazi na Viungo vyake, Mifuko ya Mayai, Uvimbe fulani, Ini,Figo,Kifuko Cha Nyonga, Maji kwenye nafasi ya Tumbo iitwayo Peritoneal Cavity na nk.

Kwa kawaida Mawimbi ya Sauti ambayo husikika na Mwanadamu huwa na Frequency kuanzia 20Hz Hadi 20000Hz (20KHz).

Ultrasound ambayo hutumika katika Masuala ya Kiafya hutengeneze Mawimbi ya Sauti ya Juu zaidi (Ultrasonic Sound Waves) yenye Frequency Kuanzia 2MHz hadi 18MHz
ambayo si rahisi kusikika na Mwanadamu katika Hali ya kawaida.

Taswira inayotengenezwa na Ultrasound huwa hafifu zaidi ukilinganisha na Taswira au Picha inayotengenezwa na Mashine nyingine Mfano X-ray au CT-Scan hii ni kwa sababu Ultrasound hutengeneze Picha kwa kutumia Mawimbi ya Sauti Wakati X-ray hutengeneze Picha kwa kutumia Miale ya Mionzi (Ionizing Radiation).

AINA MBILI ZA ULTRASOUND.
Kuna Aina Kuu Mbili za Ultrasound ambazo hufanyika Katika kipindi cha Ujauzito. Ambazo Ni;

1. Transabdominal Ultrasound.
Hii hufanyika pale ambapo Kifaa Cha kuelekeza Mawimbi ya Sauti (Probe/Transducer) huwekwa juu ya Ngozi ya Tumbo la Mjamzito baada ya Mjamzito kulala chali. Ambapo Mjamzito hupakwa Mafuta lainishi (gel) kwenye sehemu ambapo hutakiwa kuwekwa Probe, Mafuta hulainisha Ngozi vile vile hufanya Mawimbi ya Sauti kusafiri vizuri na kutengeneza picha yenye mwonekano Mwanana.

Kumbuka:
Mjamzito hutakiwa kunywa Maji angalau glasi 4 au Lita 1 Nusu Saa au Saa 1 kabla ya kufanya Ultrasound ili Kibofu Kijae Mkojo, hususani mwanzoni mwa Ujauzito au Kabla Mimba haijawa kubwa.
Kunywa Maji husaidia ktk Mambo ya Fuatayo;
1. Kibofu Kijae Mkojo Huwa kama dirisha la kupitiisha Mawimbi ya Sauti vizuri na kusaidia kuonesha Picha vizuri ya Mji wa Uzazi.

2. Kibofu Huweka Mji wa Uzazi katika Mkao mzuri ili uweze kuonekana vizuri kwenye Skrini ya Ultrasound.

3. Kibofu kilicho Jaa Mkojo huondosha Baadhi ya Viungo mfano Utumbo endapo utakuwepo Kati ya Mji wa Uzazi na Kibofu ambao unaweza kuzuia Baadhi ya vitu visionekane vyema na kwa ufasaha.

2. Transvaginal Ultrasound
Hii hufanyika pale ambapo Probe au Transducer huingizwa kwenye Njia ya Uzazi au Ukeni.
Hii inapofanyika Mjamzito hupaswa kukojoa na kuhakikisha kwenye Kibofu Cha Mkojo kunakuwa hakuna kitu kabisa tofauti na Ile inayofanyika juu ya Ngozi ya Tumbo la Mjamzito.
Aina hii ya Ultrasound hutoa Majibu sahihi zaidi ya Umri wa Ujauzito inapofanyika Miezi Mitatu ya mwanzoni mwa Ujauzito yaani Mimba yenye umri chini ya wiki 14.

3. Aina nyingine ya Ultrasound huitwa
Doppler Ultrasound, hii hutumika kuangalia Usafirishwaji wa Damu kwenye Mwili wa Mwanadamu, Mfano Usafirishwaji wa Damu kwenye Mrija unaounguanisha Kati ya Mtoto na Kondo la Nyuma (Cord) na kwa Mtoto pia.

ULTRASOUND HUWA NA MADHARA KWA MJAMZITO AU MTOTO ALIYEKO TUMBONI MWA MJAMZITO??
Ultrasound haina Madhara yoyote kwa sababu hutengeneze Picha au Taswira ya Kiungo Cha Mwili kwa kutumia Mawimbi ya Sauti tofauti na X-ray ambayo hutumia Mionzi Hatari inayotengenezwa kwa Umeme Mkubwa na hatari kwa Mtoto aliyeko Tumboni.

NB: Endapo Kuna ulazima wa kufanya X-ray kwa Mjamzito basi Utatakiwa kuvaa mavazi maalumu kwa ajili ya kumlinda Mtoto asipate athari zitokanazo na Mionzi mikali inayotengenezwa na Mashine ya X-ray.

KUNA UMUHIMU WA KUFANYA ULTRASOUND KWA MJAMZITO YEYOTE?
Ndio, Kuna Umuhimu wa kufanya Ultrasound hususani katika kipindi cha Ujauzito mfano husaidia kujua yafuatayo;

1. Kuhakikisha kama kweli wewe ni Mjamzito na Mimba iko kwenye Mji wa Uzazi au Nje ya Mji wa Uzazi hususani inapofanyika mwanzoni mwa Ujauzito katika Miezi Mitatu ya mwanzoni.

2. Kukusaidia kujua umri wa Mimba hususani kwa akina Mama ambao hedhi zao haubadiliki badiliki na Endapo Ultrasound itafanyika Miezi Mitatu ya mwanzoni mwa Ujauzito.

NB. Ultrasound ya Miezi Mitatu ya mwanzoni mwa Ujauzito huwa na usahihi mkubwa wa Umri wa Mimba na tarehe ya matarajio na huwa na utofauti wa Siku ±3 au 4 katika Umri wa Ujauzito.

3. Kuangalia Uwingi wa Maji yanayomzunguka Mtoto, Ukuaji wa Mtoto na Magonjwa, Mahari Kondo lilipo jishikiza kwenye Mji wa Uzazi au Ukilema wa Mtoto awapo Tumboni mwa Mjamzito.

4. Kukadiria Uzito wa Mtoto Tumboni mwa Mjamzito, Hali ya Kondo la Nyuma na Kujikunja kwa Mrija wa Kondo la Nyuma, Kutokukua kwa ufasaha kwa Mtoto Tumboni mwa Mjamzito.

No comments.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *