Maumivu ya Tumbo Chini ya Kitovu kwa Mjamzito Husababishwa na Nini?

Maumivu ya Tumbo Chini ya Kitovu kwa Mjamzito Husababishwa na Nini?

Maumivu ya Tumbo Chini ya Kitovu kwa Mjamzito Husababishwa na Nini?

Maumivu ya Tumbo Chini ya Kitovu kwa Mjamzito huweza kuwa Hali ya kawaida kutokana na mabadiliko mbalimbali katika kipindi cha Ujauzito au Dalili Hatarishi, Mambo yafuatayo huweza kusababisha Maumivu ya Tumbo kwa Mjamzito katika vipindi fulani fulani vya Ujauzito;

1. Mimba kujishikiza kwenye Mji wa Uzazi.
Mara baada ya Mimba kutungwa kwenye Mirija ya Uzazi,husafiri na kujishikiza kwenye Mji wa Uzazi huweza kupelekea maumivu ya kubana na kuachia kwa muda fulani na badae huacha yenyewe huhitaji Dawa.

2. Maumivu ya kubana na kuachia| Braxton Hicks Contractions
Haya ni aina ya Maumivu ambayo hutokea katika kipindi chote Cha Ujauzito inawezekana Miezi Mitatu ya mwanzoni, katikati au Miezi Mitatu ya Mwishoni mwa Ujauzito, kutokana na Ongezeko la Homoni ya Oxytocin Katika kipindi cha Ujauzito hususani nyakati za Usiku na ahsabuhi mapema, muda ambao wanawake wengi wajawazito hupata maumivu haya. Maumivu haya huwa na Tabia ya kutokea na kupotea na hujirudia rudia isipokuwa huwa haya ongezeki kadiri muda unavyoenda badala yake huweza kuacha kuuma yenyewe bila matumizi ya Dawa.

3. Mimba kutishia kuharibika au Uchungu wa Mapema.
Aina ya Maumivu tajwa hapo juu Braxton Hicks Contractions endapo yakiwa yanaongezeka kadiri muda unavyoenda huweza kusababisha Uchungu usio sahihi | Falsed labor au Hupelekea Mimba kutishia kutoka au kuharibika endapo yatakazana kuongeza na Mimba ikiwa chini ya Wiki 28 au Miezi 7, Lakini kumbuka kwamba endapo Maumivu hayo yataongezeka na Mimba iko Ina umri wa zaidi ya Wiki 28 na Chini ya Wiki 37 husababisha Uchungu kabla ya Wakati.

4. Uchungu Wa kawaida.
Endapo unapata maumivu ya Tumbo ya kubana na kuachia, na umri wa Mimba yako ni Wiki 37 hadi 42,Basi hiyo huashiria ni Dalili ya Uchungu, kwa kawaida Maumivu ya Uchungu huanza kidogo kidogo lakini huongezeka kuuma kadiri muda unavyokwenda na spidi yake huongezeka kadiri muda unavyoenda na Mwisho hupelekea Mjamzito kujifungua Mtoto.

5. Maambukizi ya Bakteria au Vijidudu kwenye mfumo wa Mkojo| UTI.
Endapo unapata Maumivu chini ya Kitovu ambayo yanatokea kipindi cha kukojoa au kutoa Haja ndogo, Homa au hamu ya kwenda haja ndogo inaongezeka Mara kwa Mara huonesha kuwa una Maambukizi ya bacteria kwenye mfumo wa Mkojo.
Hivyo unahitaji vipimo na Matibabu.

6. Mawe kwenye Mfuko wa Mkojo.
Wakati mwingine Maumivu ya Chin ya Kitovu na pembeni mwa Tumbo husababishwa na Mawe kwenye mfumo wa Mkojo, hii ni kwa sababu ya Homoni ya Progesterone ambapo hupunguza mjongeo wa Mkojo na kufanya ongezeko kubwa la Maji kwenye Figo | Hydronephrosis hii huwezi kupelekea Mjamzito kupata Mawe kwenye mfumo wa Mkojo.

Maumivu Chini ya Kitovu ktk kipindi cha Ujauzito

Response to "Maumivu ya Tumbo Chini ya Kitovu kwa Mjamzito Husababishwa na Nini?"

  • Tatizo langu mara ya Kwanza mimba ili haribika na mi ya miezi miwili baada ya wiki mbili damu ilikata na Siku tatu baadae niliingiliana na mwenzangu bila kinga lengo tupate. Mwingine lakini baada ya Siku kama tano tunagombana nikalia Sana muda kidogo tumbo linaniuma na damu ikaanza kutoka inakirangi kama cha uaridi kama mkojo nyepesi shida itakuwa ni nini ety

  • Dokta habari… mm nina maswali mawili..
    1: kama ulissx tar 6 mwez wa tatu mpk leo 27/3 unawez kusema mimba in muda gani??
    2: mm nilishawah kuona dalili za ectopic preg kweny mimba yangu ya kwanza… bahat mbay ilitoka.. je kwa muda niliokuuliza hapo naweza kwenda hospital na dokta akaigundua kam nina normal or ectopic preg

  • Sorry eti mama mjamzito anapata maumivu sana kuanzia kweny tumbo mpka kweny haja kubwa tumbo apo linamuuma sana mimba ina wiki tatu

  • Habari Dr. nina week 39 kwa sasa na nina fungal infection ambayo imeshaanza kuwa treated na kuna maji meupe yanatoka ukeni na kuchuruzika mtoto anacheza vizuri. Sasa maumivu yanayonipata chini ya tumbo (kama period) kuzunguka kiuno hadi Mgongo ni uchungu au ni hii infection?

  • Samahani sijapim mimba Ila nikama ninayo maam matiti yamekua meusi Sasa tatizo kichwa kinauma Kila siku asubui na tumbo la chini je nifanyaj au nimeze daw gan

  • Samahani dr mimi nna mimba ya miez mitatu ila naumwa chini ya tumbo nkikala upande kugeuga n shida kiungio cha mapaja na sehem za siti zinauma nkitaka kujigeuza au kushuka kitandani na kuna siku iliashawai toka kidogo je tatizo n nn dr

  • Doctor mimi nina miez mi wili ila naelekea wa 3 nasumbuliwa na UTI haziishi sijuh nisugu nimetumia mpka sindano nikiwa na mimba mwezi mmoja lakini bado

  • Poleni sana kwa gote hayo lakini cha muhimu nendeni hospitali kwani majibu sahihi ni vipimo tu

  • Nina mimba ya week 8 lakini naumwa kila siku tumbo la chini kama la period huu ni mwezi sasa linauma kila siku na matiti bado yanauma kama dalili za period kuna muda naumwa mgongo pia nin shida

  • Habari yako dokta naomba nikuulize juzi tarehe 9/9/23 nilienda kumpima mkewangu afya akakutwa na malaria na UTI kisha nikwaomba wampime na UTP ili tujue ana mimba maana hedhi yake hakuiona ktk yale masiku aliyoyazoea bahati nzuri ameonekana mimba anayo.sasa dkt mpaka sasa mkewangu analalamika tumbo lamuuma sana Chini ya kitovu

  • Hi mamaafya mke wangu ana ujauzoto wa wiki nne na upatwa maumivu makali chini yakitovu
    na kiuno ambayoo uweza kudumumu siku nzima. Ili husababishwa na nini.?

    • Doctor. Mimi Mkewangu Ujauzito Ulitoka Ukiwa Na Miezi Miwili.Na Nusu Nibaada Ya Kuwa Anapata Maumivu Makubwa Sana Chini Y Kitovu, Alivyoend Hospital Akaambiw Mimba Imeharibik Ndipo Wakamvuta Vikatoka Na Baad Y Kuvitoa Damu Zilitoka Nying, Na Baadaye Akawa Ametok Hospital Na Hakupew Daw Yoyote Bali Alitumia Dawa Z Maumivu.Tu, Mpk Wiki Tatu Zimeish Kukawa Kunatok Uchafu Wa Kawaid Tu! Tena Mudogo Mara Leo Usitoke Mara Utoke Mpka Nikawa Nakutana Naye Baada Y Siku Kama Sikuhiyo Hamuna Uchafu, Lakin Baad Y Mwez Kuisha Sasa Ndo Damu Nzito Za Mabonge Mabonge Zimeanz Kutoka Na Damu Nyepesi, Pia Kutokwa Na Haruf Ukeni Kila Akiend Hajandogo Vimabonge Vidogo Vilivyochanganyana Na Damu Vinatoka, Na Pia Mda Huu Sasa Ahisi Tena Tumbo Kuuma Kwa Mbali Tena Chini Ya Kitovu, Mwili Kuwa Dhaifu Maramojamoja Mara Kupenda Kula Udongo. Naomba Ushauri Doctor

  • Leave a Reply

    Your email address will not be published. Required fields are marked *