Je Mjamzito anaweza kupata Hedhi?
Je ni kweli kwamba unaweza kupata Hedhi katika kipindi cha Ujauzito?
Hapana!
Ukweli ni kwamba mara baada ya kupata Ujauzito au Mimba huwezi kupata Hedhi, Baadhi ya Wajawazito hususani wale ambao hupata Mimba kwa Mara ya Kwanza (Prime gravida) huweza kuchanganya wanapotokwa na Damu mwanzoni mwa Ujauzito na Hedhi yao!
Tafiti zinaonesha kwamba asilimia 10 mpaka 15 ya Wajawazito huweza kupata Dalili za kutokwa na Damu katika Ujauzito wao hususani Mimba inapokuwa chini ya wiki 16 au chini ya Miezi 4 ya Ujauzito.
Kutokwa na Damu katika kipindi cha Ujauzito huweza kuhatarisha Mimba yako na matokeo yafuatayo mfano;
1. Mimba Kutoka au kuharibika na hivyo kutojifungua Mtoto wako.
2. Kujifungua Mtoto kabla ya wakati.
3. Kujifungua Mtoto mwenye Uzito wa chini zaidi.
4. Kupungukiwa Damu ktk kipindi cha Ujauzito au hata baada ya kujifungua au Mimba yako kuharibika.
MAMBO YANAYOPELEKEA MJAMZITO KUTOKWA NA DAMU.
1.Mimba kutishia kutoka au kuharibika kabla ya kujifungua!
2. Kondo la Nyuma linapojishikiza kwenye Mji wa Uzazi huweza kupelekea kutokwa Damu katika kipindi Cha Ujauzito hususani mwanzoni mwa Ujauzito ambapo hutokea katika siku zile zile ambazo Hedhi ya kawaida ingetokea japokuwa huwa kunakuwa na utofauti na Hedhi ya kawaida Damu hutoka kidogo na kwa siku chache na badae hukata yenyewe.
3. Mimba kutunga nje ya Mji wa Uzazi huweza kupelekea kutokwa na Damu ktk cha kipindi Cha Ujauzito (Arias Stella Reaction) hususani mwanzoni mwa Ujauzito chini ya wiki 12 za Ujauzito kutoka na Upungufu au uzalishwaji mdogo wa Homoni ya Progesterone ukilinganisha na Mimba ya kawaida.
4. Mimba Zabibu, Mimba Zabibu kwa kawaida huwa lazima iharibike au itoke baada ya muda fulani wa Ujauzito hususani mwanzoni mwa Ujauzito (Chini ya wiki 16) hivyo huwesa kupelekea kutokwa na Damu katika kipindi cha Ujauzito.
5. Sababu zisizo Julikana, kuna baadhi ya Wajawazito hutokwa na Damu bila kuwa na sababu zinazojulikana au zinazopelekea kutokwa Damu katika kipindi cha Ujauzito.
KUMBUKA: Asilimia nyingi ya Wanawake wanaotokwa na Damu katika kipindi cha Ujauzito hujifungua Salama Watoto wao.
Usikose kutembelea video hii kuhusu kupata Hedhi katika kipindi cha Ujauzito.
Response to "Je Mjamzito anaweza kupata Hedhi?"
Helo
Hiyo hali imenitokea na sijui nifanye je
Nimeenda hispital nimechek utrasound inaoneksna mimba ni ndogo sana
Sasa na hii hali ya kupata hedhi ndo kabisa imenivuruga
Mchumba wangu kapima kakutwa na mimba ya miezi3.5 na hedhi katika miezi hiyo kapata nataka kujua je , kuna uwezekano wakuwa na mimba na ukapata hedhi ? Maana kaambiwa ipo nje ya kizazi na je kunamadhara gani ikiwa hivyo na tiba yake nini?
Soma hapo juu vizuri
Ulijifungua salama maana hii hali inanisibu hata mm
ok
Hi.
I have the same case… until now am not sure if the baby is still alive..at first, (before getting pregnancy) I got overbleeding I don’t know if this situation of getting bleeding is due to overbleeding I had before.
Go to hospital for more investigation
Io kipindi nakipitia sai maadamu nimepata maelezo nitakimbia hospitali maana imenikoroga sana akili jambo hili na mimi ni mjamzito wa mwezi moja
Pole sana
Mimi nina dalili zote Za mimba ila damu imetoka leo asubui ila sio nying na inaendelea kutoka je nikinunua upt nipime itasoma au niende ultrasound tu
Pima Mimba haina haja ya ultrasound
Hello, wife wangu alikuwa au anatumia siku 4 kubleed lakini alipokuwa siku za hatari nilikutana nae , Cha ajabu muda wake wa hedhi ulipofika mwezi huu kableed siku 1 tu ikakata Sasa je huenda Ana mimba Changa au ikoje kitabibu? Nisaidie majibu ikiwezekana nitumie kwa 0764189966 au email _milembeulimwengu@gmail.com
Naomba afanye kipimo cha Mimba cha mkojo
Habari nimepima jumamos kipimo kina mistari miwili leo nimeamka asubhi nikafanya tendo la ndoa mda wa 3 naona hedhi .. ni nini tatizo?
Sijakuelewa ndugu yangu
Je ni kweli mtu akiwa na mimba na akableed mimba inapungua? Kama amebleed miezi 2 basi atajifungua baada ya miezi 11 badala ya miezi 9?
Hapana ndugu yangu
Nilitumia p2 baada ya tendo maana ilikuwa siku za hatari ila nimepata hedhi kwa wakati na hakukuwa na mabadiliko ya siku kupungua au kuzidi ni zilezile siku tatu ila sasa baada ya wiki mbili napata kichefuchefu tumbo kujaa gesi na uchovu je ni madhara ya p2 au ujauzito??
Mabadiliko ya kawaida hakuna shida yoyote ndugu yangu
Natokwa na damu nanina maumvu pia nihatari?
Ndio
Kuna mdada latiba imebadilika ana anzia 21 je? Niwakati gani sahihi kupata mimba?
Sijakuelewa
Jamani Mimi nilipima nikagundua nina ujauzito lakini toka nimepima nikawa nimeona dalili za hedhi nikaenda hospital nikapima nikapatiwa dawa ila Cha kushangaza adi leo ni siku ya kumi niko hedhi shida ni nini
Mimba itakuwa imeshaharibika
Kipindi mpenzi wangu sijagundua ana mimba nilijua anasumbuliwa na magonjwa mengine akawa anatumia madawa vp izo dawa zinaweza kualibu ujauzito
Mimi sifahamu dawa alizokuwa anatumia mpeleke hospitali
Mm nilipima na kipimo kinaonesha kuwa nina mimba ila nashangaa Nina maumivu ya tumbo makali sana na nimetokwa damu kwa ck zisizo pungu 9 je hii Ina maana gana doctor?
Inawezekana inatishia kuharibika ni vema uende hospitali wakufanyie uchunguzi.
sasa mfano nimepata mimba uku damu zikatoka mi nikajua bleed kumbe sio ni kwa namna gani ntaweza kujua kam nin mimba
Tafadhari soma vizuri hapo juu
Jee mtu kubleed akiwa na mimba yaiezi sita inaashiria nini
Soma vizuri hapo juu