Je ni Mambo gani hufanya Mtoto kutogeuka Tumboni mwa Mjamzito??

Je ni Mambo gani hufanya Mtoto kutogeuka Tumboni mwa Mjamzito??

Je ni Mambo gani hufanya Mtoto kutogeuka Tumboni mwa Mjamzito??

Mtoto hugeuka yaani hugeuza chini Mimba inapofikisha wiki 32 hadi wiki 36 mabadiliko haya huwa ya asili, Mtoto anaweza kuwa ametanguliza Matako au Makalio pamoja na Miguu Mimba ikiwa haijafikisha wiki 36 hali hiyo huwa ni kawaida kabisa kwa sababu anaweza kugeuka na kugeuza kichwa chini tayari kwa ajili kutoka Mimba inapofikisha wiki 36 na kuendelea.

KUMBUKA: Mtoto huweza kugeuka mpaka wiki 36 hii hutokana na vile Mtoto anavyocheza Tumboni endapo kuna Maji ya kutosha kwenye Mji wa Uzazi (Amniotic fluid), Ifikapo wiki ya 36 Mtoto haitakiwi ageuke upande wowote na hubaki kwenye mkao huo huo Kiasili.
Hivyo kama Mimba yako imefikisha wiki 36 au zaidi na Mtoto amegeuza Matako basi hakuna uwezekano wa kugeuka Tena mpaka kujifungua kwako wewe Mjamzito.

MAMBO YANAYOPELEKEA MTOTO KUTOGEUKA TUMBONI MWA MJAMZITO.
Mambo yafuatayo huweza kupelekea Mtoto kutogeuka Tumboni mwa Mjamzito na Mtoto hutanguliza Makalio mpaka Muda wa kujifungua, Mambo yamegawanyika katika makundi Matatu ambayo ni:-

1. SABABU ZA MAMA (MJAMZITO) MWENYEWE.
Hii huweza kupelekea Mtoto kutogeuka Tumboni kwa Wakati kutoka na Mama mwenyewe mfano;

I). Mama aliye jifungua Mara nyingi,mfano zaidi ya Mara 5 huwa na Tumbo ambalo limelegea sana hii huweza kupelekea Mtoto kutogeuka Tumboni mwake wakati ambao alitakiwa kugeuka na kujiandaa kuzaliwa na Mjamzito kujifungua

II). Mjamzito mwenye ulemavu wa Nyonga mfano; Mama mwenyewe Nyonga ndogo au isiyojitosheleza kuweza kujifungua kawaida huweza kupelekea Mtoto kutogeuka Tumboni mwake.

III). Mjamzito mwenye Uvimbe (Fibroids) kwenye Mji wa Uzazi huweza kuzuia Mtoto kugeuka katika kipindi ambacho alitakiwa kugeuka ili kuzaliwa.

2. SABABU ZA MTOTO ALIYEKO TUMBONI MWENYEWE.
Inawezekana Mjamzito hana shida yoyote ila kuna sababu kutokana na Mtoto aliyeko Tumboni mwa Mjamzito ndio anapelekea kutogeuka kwa wakati Kama;

I). Mimba ya Watoto Mapacha, endapo wako Watoto wawili au zaidi Tumboni inaweza kupelekea Mtoto mmoja kutanguliza Makalio.

II). Mtoto aliyezaliwa kabla ya wakati huweza kutokuwa hajageuka kwa sababu amezaliwa kabla wakati na tafiti zinaonesha kwamba,

a. 20% ya Wajawazito wanapofikisha Wiki 28 za Ujauzito Watoto huwa wanakuwa wametanguliza Makalio.

b. 5% ya Wajawazito wanapofikisha Wiki 34 za Ujauzito Watoto huwa wanakuwa wametanguliza Makalio.

c. 3% – 4% ya Wajawazito wanapofikisha wiki 37 hadi Wiki 40 za Ujauzito Watoto huwa wanakuwa wametanguliza Makalio.

III). Mtoto mwenye Kichwa kikubwa | Hydrocephalus au Mtoto asiyekuwa na Fuvu au Fuvu lisilokamilika.

IV). Mtoto aliyefia Tumboni

V). Down Syndrome, Patau Syndrome na Edwards Syndrome.

3. MAJI YALIYOKO KWENYE MJI WA UZAZI AU KONDO LA NYUMA.

I). Maji mengi kwenye Mji wa Uzazi au Maji Machache kwenye Mji wa Uzazi huzuia Mtoto kutogeuka kwa wakati.

II). Kondo la Nyuma kujishikiza karibia na Mlango wa Uzazi au Kujishikiza sehemu ya juu kwa pembeni karibia na maungio ya Mirija ya Uzazi.

III). Mrija mfupi unaoungunisha Kondo la Nyuma na Mtoto huweza kuzuia Mtoto kugeuka katika Mji wa Uzazi na Mtoto kutanguliza Makalio/Matako.

Usikose kutembelea YouTube pale

Unaweza kunifuatilia kwenye channel YouTube.

No comments.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *