MJAMZITO HUTAKIWI KUMEZA SP ZA MALARIA MIEZI MITATU YA MWANZONI MWA UJAUZITO!

MJAMZITO HUTAKIWI KUMEZA SP ZA MALARIA MIEZI MITATU YA MWANZONI MWA UJAUZITO!

MJAMZITO HUTAKIWI KUMEZA SP ZA MALARIA MIEZI MITATU YA MWANZONI MWA UJAUZITO!

Sulfadoxine-Pyrimethamine (SP) ni dawa za Malaria hupatikana kwa Jina la Fansidar au Orodar ambazo hutolewa kwa Wajawazito kuanzia Mimba inapofikisha Miezi mi4 kwenda juu kulingana na andiko la mwaka 2012 la shirikia la Afya Duniani (WHO).

Dawa hizo hazitakiwa kutumiwa kwenye Miezi Mitatu ya mwanzo ya Ujauzito kwa sababu ya athari zake ambapo huzuia uchukuwaji/Matumizi ya folic acid kwa baadhi ya vimeng’enyishi au vilainishi ambavyo huhusika na kutengeneza Visaba ambavyo ndivyo huhusika katika utengenezwaji wa viungo mbalimbali vya Kijusi/Mtoto anapokuwa tumboni hususani katika kipindi cha Miezi mitatu ya Mwanzo ambapo kuna uhitaji mkubwa wa vitamin hizo ambazo ni Folic acid.

Ufanyaji kazi wa Dawa za SP huingilia kazi hiyo ya utengenezwaji wa Vinasaba ambapo hutumia rasimali Folic acid ambapo vimeng’eshi vya Mwanadamu hutumia folic acid kama vile vimeng’eshi vilivyomo kwa Plasmodiamu na kumfanya Plasmodiamu kushindwa kuishi na kufa,

Pamoja na kuteketeza Plasmodiamu hao na Dawa hizo huweza kuleta madhara kwa Mwanadamu hususani katika kipindi cha Miezi 3 ya Mwanzo ya Ujauzito.

Mjamzito hairuhusiwi kutumia SP za Malaria katika kipindi cha Miezi Mitatu ya Ujauzito.


Response to "MJAMZITO HUTAKIWI KUMEZA SP ZA MALARIA MIEZI MITATU YA MWANZONI MWA UJAUZITO!"

    • Kama umetumia basi unakuwa hamna namna ni vema kutumia folic acid zaidi kwa sababu hizo Dawa huingilia na kuharibika ufanyaji kazi au uchukuliwaji wa folic acid katika Mwili na kufanyika kwa vinasaba.

  • Leave a Reply

    Your email address will not be published. Required fields are marked *