JINSI YA KUNYONYESHA MTOTO NA FAIDA ZAKE!
KUNYONYESHA hii ndio njia bora ya kumpa Maziwa yako kama Chakula kwa Mtoto wako Mchanga ili aweze kukua Kiakili na maendeleo yake kiafya.
Kulingana na Shirika la Afya Duniani(WHO) na Shirika la Watoto Duniani (UNICEF) yanapendekeza Mama aliyejifungua Mtoto Mchanga kufanya yafuatayo;
- Kumnyonyesha Mtoto Mchanga mwenye umri wa chini ya Miezi 6 Maziwa ya Mama pekee bila kuongeza vinywaji vingine hata Maji au Vyakula vingine isipokuwa tuu kama Mtoto huyo amepata Ugonjwa fulani anaweza kupewa maolo(ORS) au Matone ya Vitamini, Madini au Dawa fulani.
- Mama hutakiwa kumuanzishia Mtoto vyakula vya hali ya kimiminika mfano Uji, Mchuzi wa nyama wakati ambapo pia Mtoto ataendelea kunyonya Maziwa ya Mama mpaka afikapo umri wa miaka 2 au zaidi.
MAMA AMBAYE UMEJIFUNGUA KUMBUKA MAMBO YAFUATAYO;
Ili Mama uweze kuhakikisha mwanao ambaye ni Mchanga anakuwa na ukuaji kiafya unatakiwa kufuata maelekezo haya:
- Ni vema Mara baada ya kujifungua tuu uhakikishe unamgusisha mwanao kwenye mwili wako yani kunakuwa na mgusano wa ngozi yako na ya Mtoto na umnyonyeshe Mtoto Mara tuu baada ya kuzaliwa au ndani ya saa moja tokea umejifungua.
Kitendo cha Mtoto wako kugusana ngozi kwa ngozi na wewe inaonesha wazi Mtoto wako Yuko vizuri hahitaji usaidizi wa kupumua Mara baada ya kuzaliwa!
Mtoto Mchanga anatakiwa kuwa mkavu muda wote hivyo endapo kuna nepi au Pampasi zimelowa mbadilishe mapema endapo atabaki kwenye unyevu huweza kupelekea Mtoto kupoteza Joto.
Kwa kawaida Mtoto huweza kujishikiza mwenyewe vizuri kwa Mama yake isipokuwa tuu Mama mwenyewe anaweza kusaidia kusogeza Mtoto huyo kuwa karibu naye au kwenye ngozi ya Mwili wake.
Haishauliwi Mama kukaa mbali na Mtoto isipokuwa endapo Mama aliyejifungua au Mtoto Mchanga anashida za kiafya
- Epuka kumpa Mtoto vyakula au Maziwa mengine kwa Mtoto wako ambayo Mchanga tofauti na Maziwa yako Mara tuu anapozaliwa kutokana na sababu zifuatazo;
a. Unapo mpa mwanao maziwa mengine baada tuu ya kuzaliwa huathiri Mtoto kuweza kunyonya na wakati mwingine Mtoto Mchanga huweza kuacha kunyonya Maziwa ya Mama aliyejifungua.
b. Maziwa ya mwanzoni ya Mama (Colostrum) ambayo huwa na rangi ya njano huwa na madini mengi, Antibodi ambazo huwa ni Kinga ya kuua Vijidudu ambao wameweza kuingia kipindi Mtoto alipokuwa anazaliwa lakini pia Maziwa haya huuandaa Utumbo kwa ajili ya kupokea Vitamini na Madini kutoka kwenye maziwa ya Mama.
- Hakikisha Mtoto amekaa vizuri kwenye kifua chako na ameng’ata vizuri Ziwa lako kipindi ambacho unanyonyesha.
Mtoto anapokaa vizuri hii husaidia mwanao kupata maziwa ya kutosha na huondoa athari mbalimbali za kiafya mfano Mtoto anaposhikwa vibaya huweza kusababishwa Mtoto kunyonya Maziwa yakiambatana na hewa hivyo Mtoto huwa na hewa au gesi nyingi Tumboni na kufanya aanze kulia kutokana na Maumivu ya kutokana na gesi kujaa Tumboni.
Lakini pia kutokana na gesi kujaa Tumboni Mtoto Mchanga anaweza akabeua Maziwa yote na Mwisho wa siku hawezi kushiba ipasavyo kwa sababu Maziwa huyarudisha yote.
JINSI YA KUMSHIKA VIZURI MTOTO WAKO KIPINDI CHA KUNYONYESHA FANYA MAMBO YAFUATAYO:
Unatakiwa kuhakikisha kwamba unakuwa umetulia na umerelaxi.
Namna ya kumshika mwanao kabla ya kuanza kumshikiza kwenye Ziwa lako ili aweze kunyonya vizuri na kushiba. unaweza kujifunza kupitia picha hapa chini.
Namna ya kuwashika Watoto wachanga wawili au Mapacha wakati wa kunyonyesha ni kama inavyoonesha picha hapo chini;
HATUA ZA JINSI YA KUMSHIKIZA MWANAO AU MTOTO MCHANGA KWENYE ZIWA LAKO
Hatua za kumshikiza Mtoto Mchanga ili aweze kunyonya kwa ufasaha ni kama ifuatavyo;
- Msogeza Mtoto wako mpaka Pua yake iwe karibu na chuchu yako
- Hakikisha Kichwa cha Mtoto wako anainua kiasi fulani ili Mdomo wa juu ugusa chuchu yako ili kumsaidia mwanao kufungua kinywa chake zaidi.
- Wakati Mdomo wa Mtoto wako uko wazi, Msogeze zaidi kwenye Ziwa lako.Lengo Chuchu yako kugusa sehemu ya juu ya ndani kinywa Cha Mtoto wako.
- Hakikisha Mtoto ameng’ata sehemu kubwa ya Chuchu yako na sehemu kubwa ya areola (eneo lote la sehemu nyeusi ya ziwaa) inapaswa kuwa ndani ya Mdomo wa mtoto wako.
- Hakikisha Mtoto wako ameng’ata vizuri na kidevu chake kimegusa kwenye ziwa lako.
- Pua ya Mtoto wako inapaswa kuwa wazi ili kumruhusu Mtoto kupumua kirahisi. Kwa kwa sababu Watoto wachanga hutumia pua wakati wa kupumua.
- Hakikisha Mtoto anapumua vizuri, endapo atakosa Pumzi huweza kupelekea kuacha kunyonya.
- Endapo Mtoto wako amejishikiza vizuri ataweza kunyonya, kumeza na kupumua vizuri. Mtoto atakavyakuwa ananyonya vizuri ndivyo anavyoweza kushiba bila kupata shida yoyote Mfano kujaa kwa gesi Tumboni
- Mtoto atakuwa amejishikiza vizuri endapo eneo lenye weusi au areola ya Ziwa lako itaonekana juu ya Mdomo wa juu wa Mtoto kuliko Chini ya mdomo wa chini wa Mtoto.
- Mashavu ya Mtoto huonekana yamejaa na utasikia na kuona Mtoto akimeza maziwa.
Unaweza kujifunza kwa kupitia picha hapo chini
Vile vile unahitaji kuinua maziwa yako kwa kushika katika mfano wa C ambayo huundwa na vidole vinne vya Mikono na Kidole Gumba kimoja kama inavyooneka kwenye picha hapo chini.
- 4.Mnyonyesha Mtoto Maziwa kila muda ambapo Mtoto anaonesha dalili za uhitaji wa kunyonya, Mtoto huhitaji kunyonya kila baada ya masaa Mawili.Mtoto Mchanga hana ratiba ya kunyonya muda wowote utahitaji kunyonyesha Mtoto wako.
Ukiona Mtoto anaonesha Dalili hizi ujue ana njaa na anahitaji kunyonya
- Kugeuza kicha upande mmoja na mwingine na kufungua Mdomo akiwa kama anatafuta tafuta kitu fulani (Rooting)
- Kulamba lamba Mdomo na Ulimi.
- Kupelekea peleka vidole kwenye Mdomo au kunyonya Vidole.
- Kuchezesha Mikono au Miguu.
- Kuchezesha Kichwa
KUMBUKA: Kulia kwa Mtoto Mchanga huwa ni dalili ya njaa zaidi wakati mwingine Mtoto anapo achwa na kulia muda mrefu huweza kulala na kushindwa kunyonya baada ya kusogezwa kwenye Ziwa badala ya kunyonya.
- Hakikisha Mtoto ananyonya Ziwa moja mpaka liishe ndipo mhamishie kwenye Ziwa lingine.
Umuhimu wa kumaliza maziwa yote ni kwa sababu maziwa ya Mwishoni huwa na Mafuta mengi ambayo husaidia katika ukuaji wa akili na kimwili, kwa hiyo muda mchache tokea umejifungua hakikisha Mtoto ana maliza maziwa yote kwenye Ziwa moja kabla ya kumhumishia kwenye Ziwa jingine. - Mnyonyesha Mtoto hata wakati wa Usiku ni muhimu sana Mtoto anahitaji kunyonya zaidi ya Mara 10 ndani ya Masaa 24.
Mama hutakiwi kabisa kutonyonyesha usiku kwa sababu Mtoto anaponyonya usiku Homoni ya prolactin hutolewa zaidi kipindi cha usiku endapo Mtoto atanyonya, Kumbuka endapo Mtoto amezaliwa siku za hivi karibu unatakiwa kumuamsha na kumnyonyesha kwa sababu vichanga kwenye siku za mwanzoni hulala zaidi hivyo Mtoto anatakiwa kunyonyeshwa angalau kila baada ya masaa 3 kwa usiku. - Epuka kumpa maziwa kwa kutumia Kopo.
Jinsi Maziwa yanavyotolewa huwa ni tofauti ukilinganisha kumpa Mtoto kwa njia ya Kopo au Matiti yako hivyo Baadhi ya watoto huchanganyikiwa endapo utaanza kuwapa maziwa ya Kopo mapema katika umri wao kitu ambacho siyo kizuri. - Epuka kumwongezea vyakula lishe katika kipindi cha Miezi 6 ya mwanzoni tokea Mtoto wako azaliwe.
Maziwa huwa na 87% ya maji hivyo huhitaji kumpa Mtoto Chini ya Miezi maji hata kama unaishi mazingira ya Ukame au Jangwani.
Si vizuri kumpa Mtoto Maziwa ya Kopo kwa sababu Baadhi ya maziwa ya Kopo huwa na Maziwa ya Ng’ombe ambayo hupelekea aleji kwa Baadhi ya Watoto wachanga.
UTAJUAJE KUWA MTOTO WAKO ANAPATA MAZIWA YA KUTOSHA NA AKUA KIAFYA?
Endapo una mnyonyesha Mtoto Maziwa vizuri na yakutosha na Mtoto anakua kiafya unataona Mambo yafuatayo:
- Mtoto ataongezeka Uzito ipasavyo:
Mtoto Mchanga mwenye Afya bora hupungua Uzito kwa 5% hadi 7% ya Uzito aliozaliwa nao Mara baada ya kuzaliwa mpaka wiki 2 halafu baada ya hapo Mtoto huanza kuongezeka Uzito kwa kati ya gramu 25 hadi 35 kwa siku. - Mtoto atakuwa anakojoa na kuloanisha Pampasi 6 kwa siku moja au Ndani ya masaa 24.
- Mtoto anakuwa anapata choo Mara 2 au zaidi ndani ya Masaa 24.
BAADHI YA AKINA MAMA HUHISI WATOTO WATOTO WAO HAWAJASHIBA ENDAPO WATOTO WAO WACHANGA WAKIFANYA MAMBO YAFUATAYO KITU AMBACHO SI KWELI.
- Mtoto kunyonya Mara kwa Mara au Kunyonya kwa muda mrefu (Dalili hii huonekana kipindi ambacho Mtoto anakuwa na ukuaji wa haraka zaidi mfano anapokuwa na wiki 3, wiki 6 na Miezi 3)
- Mtoto kuonesha dalili za njaa kali muda mfupi baada ya kunyonya ipasavyo.
- Matiti ya Mama kuwa laini zaidi.
- Mama kuto toa Maziwa mengi.
- Mtoto Mchanga mwenye tabia ya kudeka sana.
Response to "JINSI YA KUNYONYESHA MTOTO NA FAIDA ZAKE!"
HABARI ZA MAJUKUMU?
MI NAOMMBA KUULIZA. JE, NI VYAKULA GANI VINAYOMSAIDIA MAMA KUPATA MAZIWA KWA WINGI?