Je Maumivu ya Tumbo kwa Mjamzito husababishwa na Nini?
Maumivu ya Tumbo kwa Mjamzito ni jambo ambalo haliepukiki katika kipindi cha Ujauzito, Maumivu ya Tumbo kwa Mjamzito huweza kutokana na sababu za Ujauzito au Sababu tofauti na Ujauzito ambapo huweza kutokea hata kwa Mwanamke asiyekuwa Mjamzito.
Endapo Mjamzito akipata Maumivu ya Tumbo ya ghafla anatakiwa kuwahi Hospitali kupata huduma za Kitabibu kwa sababu huweza kuathiri Afya ya Mjamzito au Mtoto aliyeko Tumboni mwa Mjamzito.
Ukweli ni kwamba Dalili ya kuwa na Maumivu ya Tumbo kipindi cha Ujauzito huwa haiepukiki kwa Mjamzito yoyote katika Vipindi tofauti tofauti vya Ujauzito.
Ziko sababu nyingi zinazosababisha Mjamzito kupata Maumivu katika kipindi cha Ujauzito, Sababu hizo ni kama;
1. SABABU ZINAZOPELEKEA MAUMIVU YA TUMBO KWA MJAMZITO KUTOKANA NA MABADILIKO YA KAWAIDA YA UJAUZITO.
Mabadiliko hayo ni kama yafuatayo;
(a). Maumivu kutokana na kuvutika Mishipa inayopatikana pembeni mwa Mji wa Uzazi, ambapo hutokea endapo Mtoto anaongezeka na kukua Tumboni ambayo husababisha Maumivu ya kubana na kuachia au Maumivu, Mfano wa kitu chenye ncha Kali na kukata kata.
(b). Maumivu ya Tumbo kutokana na Maumivu ya kubana na kuachia, ambapo hutokea kwa ajili ya mabadiliko ya Homoni katika kipindi chote cha Ujauzito.
2. SABABU ZINAZOPELEKEA MAUMIVU YA TUMBO KWA MJAMZITO KUTOKANA NA MATATIZO YASIYO HUSIANA NA MJAMZITO.
Mabadiliko hayo ni kama yafuatayo;
(a). Mimba kutishia kutoka au kuharibika huweza kuchangia Maumivu kwa Mjamzito kwa asilimia 40 hadi 75, Mimba kuharibika au kutishia kutoka huchangia kiasi kikubwa cha Maumivu katika kipindi cha Ujauzito.
(b). Mimba kutunga nje ya Mji wa Uzazi, Hii huweza kupelekea Maumivu ya Tumbo kwa Mjamzito na huweza kuathiri Mimba 1 katika Mimba 60 au Mimba 1 katika Mimba 250
(c). Kupata Uchungu wa mapema au kabla ya kufikisha miezi 9 ya Ujauzito huweza kupelekea Maumivu katika kipindi cha Ujauzito.
(d). Kondo la Nyuma kuachia kabla Mimba kukomaa au Kabla ya kujifungua huweza kupelekea Maumivu katika kipindi cha Ujauzito na kutokwa na Damu.
(e). Kujikunja kwa Uvimbe ambao umejifungua katika kikonyo kilichoungana na Mfuko wa Uzazi.
(f). Mabadiliko ya Uvimbe kutokana na Kupungua kwa Damu katika Uvimbe huo kipindi cha Ujauzito.
(g). Maumivu ya Tumbo kutokana na Maambukizi ya vijidudu katika mfumo wa Mkojo.
(I). Maumivu ya Tumbo kutokana na Tumbo kujaa gesi au kufunga kwa choo ambapo hupelekea kuziba kwa Utumbo wa chakula.
KUMBUKA; Endapo Mimba yako imekomaa au kukaribia muda wa kujifungua hivyo muda wowote Dalili za Maumivu ya Uchungu huweza kuanza aina hii ya maumivu hufanana na maumivu ya kubana na kuachia isipokuwa tuu, Maumivu hayo huongezeka kadiri muda unavyokwenda na pia hujirudia rudia Mara kwa Mara kwa kadiri muda unavyokwenda.
Endapo unapata maumivu wakati wa Ujauzito unatakiwa kumwona Daktari kwa ajili ya Matibabu, kwa sababu Matibabu hutegemea zaidi na kipi kinasababisha Maumivu ya Tumbo vile vile hutegemeana Kati ya Mtu na Mtu.
Response to "Je Maumivu ya Tumbo kwa Mjamzito husababishwa na Nini?"
Habari mm tumbo Lang la chini Lina fura alaf linajaa ges tumbo na kujamba ninja siku ya kumi na mbili sijpt choo na uchovu Sana asbh,nahuwa kunamuda napwata na hasira
Ukafanyiwe Vipimo hospitali
Habari Mimi mke wangu mimba imefungu miezi tisa bado taree tu lakini ana lalamika tumbo kuhuma na anakojoa mara kwa mara na kuharisha
Hali ya kawaida kwa umri huo wa Mimba, Maumivu yakizidi mpeleke hospitali kwa uchunguzi zaidi
Habari Mimi mke wangu mtoto alicheza Kwa nguvu sana siku nzima lakini siku iliyofata amekua akisikia maumivu makali misiri ya uchungu na mtoto anacheza pole pole sana
Poleni sana naomba mpeleke hospitali
Jambo mke wangu alalamika tumbo kuuma na iko na miezi sita kuelekea saba sai
Umesoma vizuri hapo juu mkuu?
Habari mm Mimba yang ina miezi nane na wik mbil lkn ninaumwa na tumbo la Chini ya kitovu sasa sijui kama ni dalili za uchungu au
Soma hilo somo vizuri
Mkewangu anamimba ya miezi 3 ila nyama zatumbo zinamuuma
Pole sana ndugu yangu
My wife wangu tumbo linamuuma Mara kwa Mara mimbo yake Ina miezi miwili na nusu but amekuwa akilalamika Sana tumbo kuumaaa
poleni sana mpleke hospitali
Habari me nina mimba ya week 14 na weekend tatu Ila tumbo linauma chini ya kitu shida ni nini,?
Soma somo hili hapo juu pia uende hospitali ukafanyiwe uchunguzi
Habari mm mimba yangu Bado changa ina moezi miwili ila tumbo linaniuma sana hamu ya kula chochote sina na kichefuchefu ila tumbo linaniuma Kuna mda linakuwa sawa na Kuna mda linauma
Maudhi madogo madogo kwa Mjamzito ila uende hospitali wakufanyie uchunguzi