Je kipimo Cha Mimba huacha kuonesha kuwa Mjamzito lini?, Tokea Mimba kuharibika!

Je kipimo Cha Mimba huacha kuonesha kuwa Mjamzito lini?, Tokea Mimba kuharibika!

Je kipimo Cha Mimba huacha kuonesha kuwa Mjamzito lini?, Tokea Mimba kuharibika!

Mimba kuharibika ni Hali ambayo huwakuta 10% hadi 20% Kati ya Wanawake wote wajawazito yaani katika Wanawake Wajawazito 100, Kati ya Wanawake 10 Hadi 20 Mimba zao huishia kuharibika, 80% ya Mimba zinazoharibika, huharibika Miezi Mitatu ya mwanzo ya Ujauzito,

75% ya Mimba huharibika kabla ya kufikisha wiki 16 za Ujauzito sawa na Miezi Minne ya mwanzo wa Ujauzito.

Mara baada ya Mimba kuharibika,kwa Hali ya kawaida inatakiwa Dalili za Mimba na Kipimo Cha Mimba Cha Mkojo kuacha kuonesha kuwa wewe ni Mjamzito.
Inawezekana unajiuliza ni muda gani tokea Mimba iharibike kipimo Cha Mimba Cha Mkojo huacha kuonesha kuwa wewe ni Mjamzito bado, au Dalili za Mimba hupungua na kupotea kabisa.

Dalili za Mimba huanza kupungua na kupotea Kama ifuatavyo:
1.Kichefu chefu au kutapika kutokana na Ujauzito huanza kupungua siku 1 Hadi 5 Mara baada ya Mimba kuharibika au kutoka.
2. Maziwa kuuma Wakati kushikwa au kutoa Maji, Dalili hii hupotea baada ya siku 7 mpaka 10 tokea Mimba iharibike au kutoka kikamilifu.

3. Dalili ya kutokwa Damu ukeni hupungua kadiri siku zinavyokwenda na huchukua mpaka wiki 2 kupotea kabisa.

4. Kipimo Cha Mimba huacha kuonesha kuwa Mjamzito kuanzia Wiki 2 Hadi 4 tokea Mimba iharibike au itoke kikamilifu.

Je endapo Dalili za Mimba bado zipo kwa muda wa zaidi ya wiki 3 – 4 na kipimo Cha Mimba Cha Mkojo kinaonesha una Mimba zaidi ya wiki 4 au Mwezi 1 tokea Mimba iharibike humaanisha Nini?

Hii huweza kumaanisha Nini?
1.Kuna mabaki ya Mimba iliyoharibika yamebaki kwenye Mji wa Uzazi

2. Mimba Zabibu.

3. Saratani kutokana na hitilafu ya mgawanyiko wa Kondo la Nyuma.

Ufanye nini uonapo Dalili za Mimba bado zipo au kipimo Cha Mimba Cha Mkojo kinaonesha una Mimba zaidi ya wiki

Unatakiwa kwenda hospitali kufanya vipimo vifuatavyo.
1. Ultrasound ya Mji wa Uzazi ili kuangalia mabaki ya Kijusi.
2. Kupima uwingi wa Homoni ya HCG kwenye Damu.
3. Vipimo vingine vya Damu na Tezi ya Madini Joto.

Matibabu hutegemea zaidi na sababu gani imepelekea kuendelea kuwepo kwa dalili za Mimba Mara baada ya Mimba kuharibika au kutoka.

Kipimo Cha Mimba huacha kuonesha kuwa Mjamzito kuanzia wiki ngapi tokea Mimba iharibike!?

Response to "Je kipimo Cha Mimba huacha kuonesha kuwa Mjamzito lini?, Tokea Mimba kuharibika!"

  • Nimetoa mimba nina wiki mbili tumbo lauma na damu haitoki na nimetoa kwa njia ya kusafishwa asahiv n wiki ya 2 na siku 3 na kipimo bado kinasoma

  • Nimetoa mimba na mwezi lakini bado dalili za mimba ninazo ila nikipima kwenye kipimo cha mkojo mimba aimo kinakuja kimstar kimoja naweza kuwa na shida

  • Mimi militia Mumbai trehe 10/8 mwaka huu Ila damu ilitoka tu mabonge mabonge Mara moja hayajatoka Tena Nina mtoto mdogo na pia nmekutana na mine wangu Sasa nahisi dalili za mimba ila mume wangu alimwaga nje Mara zote

  • Kipimo Cha mimba hakionyeshi kabsa kama hipo na haipo wakati ilitoka ya miez miwili na wiki mbili pia
    Kunadalili ya maziwa kutoka hiyo unamanisha nn?

  • Nilitumia misoprostol damu Ilikata baada ya siku 11. Kwasas mate yanakuwa machungu na matiti yanajaa kama mtu anayekaribia kuingia hedhi, je hizo n dalili za mimba kuwepo?

  • Mi nlkuwa mjamzito kama wiki moja badae nkatoa damu kama siku nne nyingi Ila sikuwa na maumivu ya tumbo Ila sahv najhis kama mjamzito maumivu ya mgongo na kizunguzungu shda inaweza ikawa nn dk

      • Nlikuwa na mimba ya wik tatu sas nlikuwa naumwa sana nkatumia dawa ya kutoa ikatoka yalitoka mabonge siku Moja tu siku niliyo tumia hiyo dawa na uchafu mwusi umetoka Kam sik 6 hivi . Nlitoa tr kumi na Moja mwezi huu lkn tar 20 juz nkajarbu kupima ikaonekana bado ipo je itakuwa imetoka au bado na nifanyaje Nini naomba nisaidie ushauri wako doctor

          • Habari mama afya, mim nlijihis mjamzito baada ya week 3 ma nikapima kupitia upt nkakuta kweli ipo lakin nlikua napata maumiv sana chin ya kitovu na nkapata dalili zote za period na nlikua natoka uchafu wa brown….mara baada ya kumeza kile kidonge kimoja cha kutolea vikaanza kutoka vidam dam nlipomalizia vile vi4 dam ikatoka kwa muda wa siku 3 tu na sio mabonge ni dam ya kawaida kam hedhi na maumiv ya tumbo nliyapata sana kama ya hedhi je mimba imetoka??

  • Nimeharibikiwa mimba Kama wiki 2 zilizo pita zilianza kutoka damu baadae zikakata zikawa zinatoka kidog kido mpaka siku 4 tumbo liliuma Sana na mgongo kesho yake siku ya 5 kakatoka kajitu Kama ini Jana urefu sawa na kidole kidogo Cha mwisho baada ya hapo tumbo halikuniuma Tena .ila maziwa nikikamua yanatoa maji hayaumi ila zile dalili za uchovu kichef chefu kizungu zungu Sina . Nimepima kwenye upt kinasoma Bado imo Ila mstari ule umefifia Sana . Je inaweza ikawa ipo bado?? Msaada please

  • Leave a Reply

    Your email address will not be published. Required fields are marked *