Je Mama anaye nyonyesha anaweza kupata Ujauzito/Mimba?

Je Mama anaye nyonyesha anaweza kupata Ujauzito/Mimba?

Je Mama anaye nyonyesha anaweza kupata Ujauzito/Mimba?

Jibu Ndio!

Kuna baadhi ya akina Mama wanaonyonyesha hujishtukia tayari wana Mimba nyingine ndani ya miezi 6 tokea wajifungue hii ni kwa sababu wanashindwa kujua vigezo ambavyo vitawafanya wao wasitumie/watumie uzazi wa mpango na wasipate Ujauzito katika kipindi cha kunyonyesha hususani kwa Miezi 6 ya mwanzo ya watoto wao na wao kunyonyesha!

Hapana!

Endapo utanyonyesha na utakidhi vigezo hivyo basi inawezekana ukapunguza uwezekano wa kupata Mimba kwa asilimia nyingi sana kwa kipindi hicho.

Tafiti zinaonesha kwamba 1% – 2% ndio huweza kupata Mimba endapo watafuata na kukidhi vigezo hivi vitatu (3) ambapo huweza kuzuia uwezekano wa kupata Mimba kwa 98% – 99% bila kutumia njia nyingine zozote  za Uzazi wa mpango kwenye Miezi 6 ya mwanzo tokea wajifungue.

Je ni vigezo gani Mama anayenyonyesha anatakiwa kuwa navyo ili asipate Mimba katika kipindi Cha kunyonyesha hususani ndani ya Miezi 6 ya mwanzo.!

Vigezo unavyotakiwa kuwa navyo wewe kama Mama unanyonyesha ili usipate Mimba hali yakuwa hutumii njia yoyote ya uzazi wa mpango ni kama vifuatavyo;

1. Hakikisha Mtoto wako ana umri chini ya Miezi 6.

2. Hakikisha unanyonyesha Maziwa yako wewe Mama tu bila kuongeza maji wala Uji na nk, katika Miezi sita hii ya Mwanzo!
Unanyonyesha Mtoto maziwa yako kila baada ya masaa 2 – 4 kwa mchana na masaa 4 – 6 na Mtoto ananyonya mpaka anaacha mwenyewe!

3. Hakikisha hupati hedhi kwa maana kwamba huoni siku zako katika kipindi hicho.
Kuna baadhi akina mama wanaweza kuanza kutokwa na damu katika vipindi fulani fulani hususani mwezi 1 au 2 tokea wajifungue na hii haimaanishi kwamba ni hedhi.

Muhimu: Kitu kingine ni kwamba hakikisha kwamba Mtoto hanywi maziwa ya kununua dukani yani anategemea maziwa yako tuu!

❌Kama hujakidhi vigezo hivyo hapo juu basi kuna uwezekano wa hatari ya kupata Ujauzito kwa 1% – 10% katika kipindi hichi cha Miezi 6 ambapo unanyonyesha maziwa na hutumia uzazi wa mpango!

Ili kuepuka kupata Ujauzito basi utatakiwa kuanza kutumia njia za uzazi wa mpango wiki 3 Mara baada ya kujifungua na endapo umefikisha miezi 6 basi utatakiwa kuchagua njia ya uzazi wa mpango inayokufaa ili kuepuka kupata Mimba zisizo pangwa na mwisho wa siku kuanza kupata shida au kutoa Mimba ambayo ni hatari kwa afya yako na pia ni kosa kisheria!

Usikose kufuatilia video YouTube

Mjamzito unaweza kupata Mimba katika Ujauzito wako Kama hujakidhi Vigezo vifuatavyo!

No comments.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *