UMUHIMU WA VITAMINI B-9 (FOLIC ACID) KWA MAMA MJAMZITO.

UMUHIMU WA VITAMINI B-9 (FOLIC ACID) KWA MAMA MJAMZITO.

UMUHIMU WA VITAMINI B-9 (FOLIC ACID) KWA MAMA MJAMZITO.

Vitamin B-9 ni aina ya Vitamini muhimu Sana katika Mwili wa Mwanadamu na hujulikana kwa jina la Folic acid au Folate.
Neno “folic” linatokana na neno la Kilatini folium (ambalo linamaanisha jani) kwa sababu lilipatikana kwenye Mboga za Majani zenye kijani kibichi.

Kutokana na kwamba Mwanadamu mwili wake hauwezi kujitengenezea Vitamini hii wenyewe, ndio maana ni muhimu kuweza kupata Vyakula vyenye Vitamini hii ilikuweza kusaidia Mwili kupata Vitamini B-9 hii ili kuweza kuondokana na Dalili za Upungufu au umuhimu wa Vitamini hii katika Mwili.

Kwa kawaida uasili wa Vitamini hii huitwa Folate na endapo Vitamini hii ikitengenezwa huwa katika mfumo wa folic acid ambayo inakuwa na uwezo mkubwa wa kuhimili Joto ukilinganisha na Vitamini asilia ambayo huitwa Folate.

Vitamini hii huwa ya Muhimu zaidi katika Mwili kwa sababu husaidia katika utengenezwaji wa Vinasaba vinavyohusika katika utengenezwaji wa Seli hai Nyekundu za Damu, vile vile husika katika utengenezwa wa Vinasaba ambavyo hutumika katika utengenezwaji wa kiungo ambacho huhusika katika utengenezwaji wa Mfumo wa Fahamu ( Ubongo na Uti wa Mgongo) na ufungaji mzuri wa Fuvu la Kichwa na Uti wa Mgongo katika ukuaji wa Kijusi Tumboni mwa Mjamzito hususani mwanzoni mwa Ujauzito.

Usikose kutumbelea video hii pale YouTube

UPUNGUFU WA VITAMINI B-9(FOLATE) KWA MAMA MJAMZITO NA WANAWAKE WENYE UMRI KATI YA MIAKA 18 HADI 45.

Endapo Mjamzito au mwanamke mwenye umri wa miaka 18 hadi 45 amepungukiwa na Vitamin hii.
Huweza kupelekea upungufu wa Damu kwa Mjamzito mwenyewe au katika kipindi Cha Ujauzito,Vile vile huweza kupelekea Mjamzito kujifungua Mtoto mwenye Mgongo wazi au Ubongo wazi hii huweza kupelekea athari kubwa kwa Mtoto na kuongezeka kwa gharama za matitabu ili kuweza kunusuru uhai wa Mtoto wako.

Mambo yanapelekea au Visababishi vya Upungufu wa Vitamini katika Mwili wa Mjamzito au Mwanamke ni kama:

  1. Upungufu wa Vitamini katika Mlo wa kila siku.
    Kutokana na utamaduni wa jamii yetu kuto kula au kutojumisha mboga za majani za kutosha katika Milo yetu.
    Mfano;Wakati wa mchana Mwanamke anakula Ugali mkubwa kuliko Mboga Mboga za Majani au kula wali na Mboga kwa kiasi kidogo.
    Akina Mama wengi hususani Wajawazito na wale ambao wako kwenye umri ambao wanaweza kubeba Ujauzito au Mimba yaani wanawake wenye Miaka Kati ya 18 mpaka 45 huwa na Upungufu wa Vitamini hii kwa wingi katika Mili yao.
  2. Ongezeka la uhitaji wa Vitamini hii katika Mwili wa Mjamzito.
    Kwa sababu Vitamini hii huhusika katika utengenezwaji wa vinasaba ambavyo hutumika kuunda Seli hai Nyekundu za Damu na Kiungo kinachotengenezwa mwanzoni na kujifunga vizuri katika hatua za mwanzoni za ukuaji wa Kijusi Tumboni mwa Mjamzito hivyo Mjamzito huhitaji Vitamini hii Maradufu ukilinganisha na mwanamke ambaye hana Ujauzito,mwisho wa siku hupelekea upungufu wa Vitamini hii katika Mwili hususani kwa Mjamzito.
  3. Kutolewa Nje Kama taka Mwili.
    Kwa sababu Vitamini hii baada ya kutumika Mwili hutolewa Nje Kama taka Mwili kwa njia ya mkojo, hivyo wakati Mwingine hutoka au kupotea kwenye mwili kwa sababu ya kutolewa nje ya Mwili kwa njia ya Mkojo.
  4. Kushindwa kufyonzwa kutoka kwenye Utumbo kwenda kwenye Damu kutoka na shida mbalimbali kwa baadhi ya Binadamu.Hata kama umekula vyakula vyenye Vitamini hii kwa wingi.
  5. Matumizi ya Pombe kwa Mjamzito au Mwanamke ambapo Pombe huweza kuathiri ufyonzwaji wa Vitamini hii kutoka kwenye Utumbo kwenda kwenye Damu. Hata kama umekula vyakula vyenye Vitamini hii kwa wingi.
  6. Matumizi ya Dawa ambazo huweza kuzuia au kuathiri utunzwaji wa Vitamini hii katika Mwili mfano; Matumizi ya Dawa za Saratani kama Methotrexate na Dawa za kifafa kama Phenytoin, Carbamazepine na Phenobarbital.
  7. Shida zitokanazo na hitilafu ya Vinasaba
    vinavyounda baadhi ya vimeng’enyishi ambavyo huhusika katika kumeng’enya Vitamini hii na kupelekea kuto kumeng’enywa kwa Vitamini hii na mwisho wa siku kushindwa kutumika kwa Vitamini hii katika Mwili wa Mwanadamu.
  8. Upikwaji wa Mboga Mboga kwa kuunguza sana au kuchemsha muda mrefu huweza kuondoa Vitamini hizi katika Mboga hizo hata kama mboga hizo zina Vitamini hii kwa wingi.

Ukweli ni kwamba Vitamini hii hutumika zaidi chini ya wiki 3 mpaka 4 Mara baada ya Mimba kutungwa kipindi ambacho mfumo wa fahamu hufanyika baada ya hapo huwa tayari umeshafanyika hivyo Upungufu wa Vitamini hii hupelekea athari kwa Kijusi kabla ya Mjamzito kujijua au kujigundua kuwa ni Mjamzito katika kipindi kifupi Cha Mwanzoni kabisa mwa Ujauzito.

Ilikuweza kuzuia athari zitokanazo na Upungufu wa Vitamini hii ni vema kuanza kutumia Folate mapema au ikiwezekana miezi 3 hadi mwezi 1 kabla ya kupata Mimba, Hii Ni bora zaidi kwa sababu Vitamini hii hutumika kama rasilimali mwanzoni mwa Ujauzito ambapo pengine Mjamzito bado hajajingudua kuwa ni Mjamzito yaani kabla ya wiki 3 hadi 4 Ni sawa na siku 21 hadi 28 Mara baada ya Mimba kutungwa baada ya hapo endapo Mjamzito alikosa Vitamini hii tayari Kijusi chake kinakuwa kimeathirika.

NAMNA YA KUTUMIA DAWA ZA FOLIC ACID KWA WAJAWAZITO NA WANAWAKE WENYE UMRI KATI YA MIAKA 18 MPAKA 45.
Kwa sababu ya ukosefu wa Vyakula vyenye folate kwa wingi katika jamii mfano wa vyakula hivyo ni Kama;

1.Mboga za Majani mfano; Broccoli, Cauliflower, Spinach, Mboga nyingine zenye Majani ya kijani kibichi, Asparagus, Maharage na nk.

  1. Matunda mfano kama; Parachichi, Machungwa na nk.
  2. Vyakula vingine vilivyo ongezwa Folic acid kutoka viwandani mfano; Unga, Mikate na nk
    1. Shirika la Afya Duniani, WHO linapendekeza kutokana na ukosefu huo wa Vitamini hii muhimu kwa Wajawazito hususani kwenye nchi zinazoendelea kwamba,Mwanamke ambaye siyo Mjamzito ila yupo Kati ya umri wa miaka 18 mpaka 45 anatakiwa kupata angalau 400mcg ya folic acid kila siku ili atakapo pata au kupanga kuwa Mjamzito atakuwa na Vitamin hii ya kutosha mwilini mwake.
    2. Kulingana na Chuo cha Amerika cha Wataalamu wa Uzazi na Masuala ya wanawake(ACOG);Mjamzito anatakiwa kutumia Dawa za Folic acid angalau kiasi Cha 600mcg kila siku angalau kwa wiki 12 sawa na miezi mitatu ya mwanzo ya Ujauzito lakini pia kulinga na shirika la Afya Duniani (WHO) Mjamzito anaweza kutumia mpaka kiwango Cha juu kabisa Cha Dawa hizi ambapo ni 5gm bila athari zozote vile vile anaweza kuendelea kutumia zaidi ya wiki 12 za mwanzo wa Ujauzito au ikiwezekana mpaka mwishoni mwa Ujauzito wake.

Pamoja na Matumizi ya hizo Dawa unatakiwa kuhakikisha kwamba unapata Vyakula vyenye Vitamini hii kwa wingi lakini pia unaondokana na Tabia ambazo ni hatarishi ambazo zimetajwa hapo juu zitakazopelekea kuwa na Upungufu wa Vitamini hii.

Hapa nchi Tanzania Dawa hizi hupatikani kwa Majina mbalimbali na vile vile huwa na Mchanganyiko wa Vitamini nyingine lakini pia na Madini Chuma ambavyo kwa pamoja husaidia kuongeza Damu kwa Mjamzito na kupunguza shida za Mgongo au Ubongo wazi, na Dawa hizi zinaweza kuwa katika Mfumo wa Vidonge au Kimiminika na Majina hayo ni kama;

  1. FEFO hujulikana kama Ferrous Sulphate +Folic Acid huwa katika mfumo wa Vidonge.
  2. SKTONE huwa katika mfumo wa Kimiminika na huwa na Mchanganyiko wa Folic Acid, Madini Chuma na Vitamin nyingine mfano Vitamini B12 na Vitamini B6.
  3. FEROSORB huwa katika mfumo wa capsules ambayo huwa na Folic Acid, Madini Chuma na Vitamin nyingine mfano Vitamini B12 na Vitamini C na nk.

Hivyo ni vema kuweza kutumia Dawa hizo kabla ya kupata Ujauzito hususani kwa akina Dada ambao wako kwenye umri ambao wanaweza kupata Ujauzito au Miezi Mitatu kabla ya kupata Ujauzito hii husaidia kupunguza uwezekano wa kujifungua watoto wenye shida za Migongo wazi na nk kwa zaidi ya 50%!

Usikose kutembelea video hii

Vitamini B-9 kwa Mjamzito

Response to "UMUHIMU WA VITAMINI B-9 (FOLIC ACID) KWA MAMA MJAMZITO."

  • Mm nilikuwa situmii folic acid kila siku mpaka sasa mimba yangu inamiez mitano je naweza kuleta masihara Kwa mtoto

  • Leave a Reply

    Your email address will not be published. Required fields are marked *