MTOTO HUGEUKA LINI KATIKA KIPINDI CHA UJAUZITO!
Mtoto anaweza kuanza kugeuka kuanzia wiki ya 32 mpaka wiki 36
Endapo hajageuka kuanzia wiki 35 kurudi chini hiyo inawezekana isiwe shida kwa sababu anaweza kugeuka mpaka wiki ya 36 ila endapo hajageuka mpaka wiki ya 36 hiyo ndio tunaita *Breech presentation.*
*Kuna aina 3 za Breech presentation*
1. Kutanguliza miguu na matako kwa pamoja huitwa *Complete Breech*
2. Kutanguliza Matako na kukunjua miguu sehemu ya goti huitwa *Frank Breech.*
3. Kutanguliza mguu mmoja au miwili huitwa *Footling Breech*
*Je naweza kujifungua kwa njia ya kawaida Kama mtoto Yuko Breech?*
Hutegemeana mama moja na mwingine na mtoa huduma njia atakayo chagua lakini kwa siku hizi Madaktari wengi hupendelea kufanya operation (Cesarian section) ili kuepuka shida mbalimbali.
*Lakini Kuna njia ambayo Daktari anaweza fanya maneuver kwenye tumbo la Mjamzito njia hiyo huitwa _External Cephalic version_ ambayo hufanyika Kati ya wiki 36 na 38 za Ujauzito.*
Unaweza kujifunza mengi kwa kupitia video.
Mtoto hugeuka lini Tumboni mwa Mjamzito
Response to "MTOTO HUGEUKA LINI KATIKA KIPINDI CHA UJAUZITO!"
Asante kwa somo, ni zuri na nirahisi kueleweka mungu awabariki
Amina
Je mtoto akigeuka kabla ya hiyo miez mi3 ya mwisho ni tatizo?
Hapana