MICHIRIZI YA TUMBO KATIKA KIPINDI CHA UJAUZITO.

MICHIRIZI YA TUMBO KATIKA KIPINDI CHA UJAUZITO.

MICHIRIZI YA TUMBO KATIKA KIPINDI CHA UJAUZITO.

Michirizi au Mistari midogo midogo ambayo hutokea kipindi Cha Ujauzito kwenye maeneo ya Tumboni, Mapajani na kwenye Matiti ya Mjamzito,hususani Miezi mitatu ya katikati na mwishoni mwa Ujauzito, Hali huwa ni kero kwa baadhi ya akina Mama wajawazito hususani vijana au Wanawake wanaobeba Mimba kwa Mara ya kwanza hii ni kwa sababu huharibu muonekano wao wa urembo wa Tumbo.

Mabadiliko haya ya Ujauzito huwa ni ya kawaida kabisa kwa Mjamzito kutokana na:

1. Mabadiliko Mwili kutokana na ongezeka kwa Tumbo kutokana na ukuaji wa Mtoto kwenye Mji wa Uzazi wa Mjamzito au Ongezeko la Uzito kwa haraka katika kipindi cha Ujauzito.

2. Mabadiliko ya Tishu na seli zinazo iunda ngozi kwa ujumla wake.

3. Mabadiliko yatokanayo na ongezeka la baadhi ya Homoni katika Mwili mfano Homoni za cortisol na Homoni ya Relaxin ambayo hupelekea kuvunjwa kwa seli na Tishu zinayoiunda Ngozi na sababu nyingine kadhaa. Hali hii huwapata haswa Wanawake wanaopata Mimba kwa Mara ya kwanza katika Umri wa miaka 20 au katika Ujana, ambapo asilimia 48 kati yao hutokea kwenye Tumbo, asilimia 25 hutokea kwenye Matiti na asilimia 25 hutokea kwenye Mapaja.

VISABABISHI.
Vitu vinavyosababisha Mistari hii kwenye katika kipindi cha Ujauzito bado havija julikana ijapokuwa kuna vitu au Mambo ambayo yanaweza kuhatarisha kuwa na hali hii.

VIHATARISHI.
Mambo yanayoweza kuchangia au kuhatarisha kupata Michirizi katika kipindi Cha Ujauzito ni kama vile:-
1. Mimba ya kwanza katika umri Mdogo.
2. Kurithi endapo katika Ukoo fulani akina Mama Wajawazito hupata Michirizi katika kipindi Cha Ujauzito.
3. Kuwa na Uzito mkubwa kupindukia kabla au muda mfupi kabla ya kupata Ujauzito.
4. Kuongezeka Uzito kwa Kasi kubwa katika kipindi Cha Ujauzito.
5. Kujifungua Mtoto mwenye Uzito mkubwa au kupitiliza muda wa kujifungua.
6. Mimba ya Mapacha.
7. Uwepo Maji mengi kwenye mfuko wa Uzazi au Mji wa Uzazi.
8. Ngozi kuwa dhaifu kutokana na matatizo au shida zinazohusisha Ngozi.
9. Matumizi ya Madawa mfano; Corticosteroids ambayo huweza kupelekea Mistari au Michirizi huweza kutokea kwa Wanawake ambao si wajawazito.
10. Shida au Matatizo kutokana na ongezeko kubwa la Homoni za cortisol mfano; Cushing syndrome.

DALILI ZAKE:
1. Mojawapo ya dalili kubwa ni mwanamke Mjamzito kuwa na Mistari au Michirizi kwenye Tumbo, ambayo huwa na rangi ya zambarau au nyekundu (Striae Rubra) endapo ikipona au Mara baada ya kujifungua huwa na rangi  nyeupe (Striae Alba) na huweza kuwa kwenye ngozi ya chini ya kitovu au pembeni sehemu ya chini ya Tumbo lakini Wakati mwingine huweza kuhusisha Matiti kwa 25% au mapaja kwa 25% vile vile na sehemu nyingine mfano sehemu za mabegani na kwenye sehemu za juu kwenye Mikono upande wa ndani.

2. Kutokana na kuvutika kwa Ngozi Kutokana na Ukuaji wa Mtoto Tumboni mwa Mjamzito huweza kupelekea kupata dalili za kuwashwa au muwasho wa Ngozi, ijapokuwa huwa hakuna maumivu ya aina yoyote.

Hali hii huwa kama kikwazo au huleta maudhi kwa Mjamzito kwa sababu huharibu uzuri wa Tumbo la Mjamzito au baada ya kujifungua.

JINSI YA KUZUIA KUWA NA MISTARI/MICHIRIZI HII.

1. Matumizi ya vyakula vyenye Vitamini C na Vitamini D kwa wingi huweza kupunguza hali hii ya kuwa na Mistari kipindi Cha Ujauzito kwa sababu Vitamini hizi huimarisha Ngozi yako na Tishu zinayoiunda Ngozi.
2. Matumizi ya vyakula vyenye Zinki kwa wingi mfano; Matumizi ya Telele au Mbegu za Maboga.
3. Kunywa maji ya kutosha na kuepuka kutumia vinywa vyenye caffeine mfano;Soda za Pepsi, Coca-Cola na Kahawa.
4. Mafuta ya Olive, Mafuta ya Cocoa, Mafuta ya mbegu za Kungu na nk. japokuwa baadhi ya tafiti zinaonesha kwamba hakuna uhakika sana kuhusu matumizi ya haya Mafuta katika kuzuia Michirizi au Mistari katika kipindi cha Ujauzito.
5. Kupunguza Uzito mkubwa au Kiriba tumbo kabla ya Ujauzito.
6. Epuka madawa yanayo ongeza ukubwa wa Matiti.

MATIBABU.
1. Mistari hii huweza kutibiwa kwa kutumia Mafuta ya Retinoid au Tretinoin ambayo huwa na Vitamini E, Vitamini A na nk
2. Kutibiwa kwa kutumia Mionzi ambayo inaweza kusisimua ukuaji na ugawangikaji wa baadhi ya nyuzi nyuzi zinazo iunda ngozi.

KUMBUKA: MAFUTA YA RETINOID AU TRETINOIN HUWA NA MADHARA KWA MTOTO TUMBONI MWA MJAMZITO HIVYO MJAMZITO HARUHUSIWI KUTUMIA MAFUTA HAYO KATIKA KIPINDI CHA UJAUZITO LABDA MPAKA AJIFUNGUE AU MARA BAADA YA KUJIFUNGUA.

unaweza kusikiliza video kwa kubonyeza hapo chiniπŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡

Michiri kwenye Tumbo, Matiti, Mapaja na nk katika kipindi Cha Ujauzito

Response to "MICHIRIZI YA TUMBO KATIKA KIPINDI CHA UJAUZITO."

  • Asantee saana Dr.mimi ni mjamzito wa mimba ya kwanza ni miezi mitatu Sasa nasikia ngozi kama Iko na viminyoo yaani inawasha sehemu za tumbo naweza Anza kutumia mafuta ya olive oil au cocoa butter kwa sasa

  • Leave a Reply

    Your email address will not be published. Required fields are marked *