MAMBO YANAYOPELEKEA MJAMZITO KUKOSA USINGIZI NA MAMBO YA KUFANYA ILI KUPATA USINGIZI KWA MJAMZITO!

MAMBO YANAYOPELEKEA MJAMZITO KUKOSA USINGIZI NA MAMBO YA KUFANYA ILI KUPATA USINGIZI KWA MJAMZITO!

MAMBO YANAYOPELEKEA MJAMZITO KUKOSA USINGIZI NA MAMBO YA KUFANYA ILI KUPATA USINGIZI KWA MJAMZITO!

Mambo ambayo huweza kupelekea kukosa usingizi kwa Mama Mjamzito ni kama yafuatayo!

1. Kuongezeka kwa hamu ya kwenda kukojoa Mara kwa Mara usiku!

2. Kupata maumivu ya Mgongo kutokana na kulegezwa kwa ligaments kutokana na ongezeko la homoni ya Relaxin na nk.

3. Kupata Maumivu ya kubana na kauchia wakati wa usiku kwa sababu ya ongezeko la homoni iitwayo oxytocin usiku!

4. Mtoto anapocheza hupelekea wakati mwigine Mama kushindwa kulala ipasavyo!

5. Ugonjwa au shida ya kuwa na Mijongeo ya miguu wakati wa kulala usiku (RLS) kwa baadhi ya wajawazito kutokana na upungufu wa madini chuma na folic acid!

6. Kiungulia na GERD wakati wa Ujauzito na usiku.

7. Kulalia upande mmoja ambapo hupelekea Mjamzito kusijisikia vibaya au kupata maumivu wakati wa kulala husasani kuanzia miezi 7 kwenda juu.

8. Ongezeko la homoni iitwayo Estrogen ambayo hupunguza uwezekano wa kupati wa usingizi hususani miezi Mitatu ya Mwisho ya Ujauzito!

9. Matatizo au vitu vinavyopelekea Msongo wa Mawazo au shida za kisaikolojia kwa Mjamzito.

10. Kula Mlo mkubwa muda mfupi kabla ya kulala huweza kupelekea kupata kiungulia wakati wa kulala.

JINSI YA KUONGEZA USINGIZI KATIKA KIPINDI CHA UJAUZITO.
Unatakiwa kufanya Mambo yafuatayo ili kuweza kuhakikisha kwamba unapata Usingizi wa kutosha katika kipindi cha Ujauzito, Mambo hayo huitwa Tabia nzuri za kukufanya upate Usingizi (Sleep hygiene) ambayo ni;-

  1. Kulala Muda maalum unaofanana kila siku na muda wa kuamka unaofanana bila kuwa na ratiba ambayo inabadilika badilika hata kama ni mwisho wa wiki.
  2. Hakikisha chumba cha kulala kinakuwa na utulivu, Giza, sehemu ambayo unaridhika nayo pia kuwe na joto la kawaida au kiasi pasipo kuwa na baridi sana au joto sana.
  3. Usilale na simu au kifaa chochote cha kielektroniki mfano; Tv au Kompyuta.
  4. Epuka vinywaji vilivyo na caffeine mfano; Soda za Pepsi au Coca-Cola na Pombe katika kipindi Cha Ujauzito.
  5. Epuka Mlo mkubwa muda mfupi kabla ya kulala kipindi Cha Ujauzito huwa unaweza kukuletea athari mfano; Kupata kiungulia.
  6. Fanya mazoezi madogo madogo mfano kutembea tembea,kujishughulisha kama huna sababu za kuzuiliwa na Daktari.
Vitu vinavyopelekea kukosa Usingizi kipindi Cha Ujauzito na suluhisho lake.

No comments.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *