Je kwa nini Chupa hupasuka kabla ya Uchungu kuanza? | Chupa kupasuka kwa Mjamzito kabla ya Uchungu!!

Je kwa nini Chupa hupasuka kabla ya Uchungu kuanza? | Chupa kupasuka kwa Mjamzito kabla ya Uchungu!!

Je kwa nini Chupa hupasuka kabla ya Uchungu kuanza? | Chupa kupasuka kwa Mjamzito kabla ya Uchungu!!

Kwa nini kwa baadhi ya Wajawazito Chupa hupasuka kabla ya Uchungu kuweza kuanza?

Kuna Baadhi ya Wajawazito Chupa hupasuka kabla ya Uchungu kutoka na sababu mbalimbali, kabla hatujaona sababu zinazopelekea. Kuna aina Mbili kuu za Chupa kupasuka ambazo Ni;

  1. Chupa kupasuka kabla ya Mimba yako kukomaa ambapo umri wa Mimba unakuwa wiki 28 hadi wiki 36 na siku 6 kwa nchi zetu zinazoendelea Kama Tanzania, Lakini inaweza kuwa wiki 24 mpaka wiki 36 na siku 6 kwa nchi zilizoendelea.
    Kwa hivyo Chupa kupasuka chini ya wiki 37.
  2. Chupa kupasuka kuanzia wiki 37 kwenda juu mpaka wiki 42, ingawa Chupa inapasuka zaidi ya saa 1 kabla ya Uchungu kuanza.

Mambo yanayoweza kupelekea Chupa kuweza kupasuka ni Kama;

  1. Magonjwa au Maambukizi ya via vya uzazi.
    Mfano magonjwa kama Kisonono, Magonjwa ya mfumo wa Mkojo/UTI na nk.
  2. Kuongezeka kwa Udhaifu wa Kuta zinazo mzunguka Mtoto kwenye mfuko wa Uzazi.
  3. Utapia mlo kwa Mjamzito hususani Wajawazito wenye BMI chini 18.5kg/M².
  4. Shida za kurithi kutoka kizazi kimoja hadi kwa sababu ya hitilafu katika vinasaba vinavyounda Protini inayotumika kutengeneza kuta zinazo Mzunguka Mtoto.
  5. Mjamzito kuwa na Maji mengi kwenye mfuko wa Uzazi kutokana na Sababu mbalimbali.
  6. Mjamzito mwenye Mimba ya Mapacha.
  7. Mjamzito ambaye amejifungua Mara nyingi zaidi mfano kuanzia Watoto 5 na kuendelea
  8. Sababu zisizo julikana.

Dalili za Chupa kupasuka ni Kama;

Kutokwa na Maji mengi masafi ghafla au taratibu taratibu Kama matone, ni vema kuweza kuonana na watalaamu wa Afya ili kuweza kutofautisha Na Hali ya mama kujikuta amekojoa bila yeye kuweza kutambua hususani kwa baadhi ya Wajawazito kwenye Miezi mitatu ya mwisho ya Ujauzito au Maji maji ambayo huwa kama ute fulani hutoka kutoka na hali ya Ujauzito.

Matibabu hutofautiana Kati ya Mama Mjamzito Moja na Mwingine hivyo ni vema kuwahi hospital ili kupewa huduma za kiafya!

Response to "Je kwa nini Chupa hupasuka kabla ya Uchungu kuanza? | Chupa kupasuka kwa Mjamzito kabla ya Uchungu!!"

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *